Jumapili, 22 Mei 2016

Shindano la Big Brother Africa kuto fanyika mwaka 2016, Idris aendelea kushikilia taji hilo!!!


Idris Sultan 
kwa mujibu wa taarifa ya tarehe 20.5.2016 ilizotolewa na waandaaji wa shindano la BigBrother kupitia mtandao wa kijamii  www.bigbrotherafrica.com taarifa imeeleza kua shindano hilo ambalo lilitarajiwa kufanyika mwaka huu limeahirishwa hadi 2017 mwakani,

huku mshindi ambae bado anashikilia taji hilo akitangazwa kua ni Idris Sultan ambae alijipatia kiasi cha dola laki tatu baada ya kutangazwa mshindi,

taarifa hiyo imewataka wapenzi na mashabiki wa shindano hilo kuto poteza matumaini kwa kua kinachofanyika ni kuboresha zaidi na kwamba wakati utakapo wadia shindano hilo litakua katika taswira nzuri kwa washindi na wafuatiliaji (wapenzi) kwa kua maboresho yanayofanywa ni makubwa hivyo wapenzi na wadau watarajie msisimko zaidi katika shindano lijalo.

Kwa mara ya mwisho shindano hilo lilifanyika mwaka 2014



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni