Jumatatu, 23 Mei 2016
TANGAZO:AJIRA YA DHARURA KATIKA SEKTA YA AFYA
AJIRA YA DHARURA KATIKA SEKTA YA AFYA
UTANGULIZI Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeridhia mpango wa Ajira ya dharura kwa wataalamu wa fani mbili za afya. Mradi huu umelenga kuchangia juhudi za serikali katika kukabiliana na uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika sekta hii.
Mpango huu utaendeshwa kwa Fedha za mfuko wa CDC (Centre for Disease Control) Awards No. 5U2GGH001062-03 kwa mwaka wa Fedha ulioanzia Aprili 2016 kwa muda wa miaka miwili. Watumishi watakaopata ajira kupitia mradi huu wanakadiriwa kuwa 192 na watapangiwa vituo vya kazi vilivyoko katika maeneo yenye uhaba mkubwa na ambayo mazingira yake ni magumu.
Watumishi hawa baada ya kumaliza mkataba wao, wataingizwa katika ajira za serikali kulingana na upatikanaji wa vibali vya ajira kwa mwaka husika. Watumishi hawa ni kama ifuatavyo: Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant) 95 na Wauguzi (Enrolled Nurses) 97. Maombi yote yaambatanishwe kivuli cha cheti cha kumaliza kidato cha nne, cheti cha taaluma pamoja na leseni (kwa wauguzi)
MSHAHARA NA MASILAHI
Mshahara (kwa kiwango cha juu cha mshahara wa kila fani husika)
Posho ya kujikimu ya siku saba za mwanzo
Bima ya Afya ya asilimia 3%
Kiinua m,gongo cha asilimia 25% ya mishahara baada ya miaka (2);
Malipo ya pango ya asilimia 30% ya mshahara
Nafasi ya kupatiwa mafunzo elekezi.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/06/2016, Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta:-
Katibu Mkuu
Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
S.L.P 9083
6 Samora Machel Avenue, 11478
Dar es salaam, Tanzania
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni