![]() |
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini Geneva-Uswis |
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache
katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia
la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee
na watoto Ummy mwalimu wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani
unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.
Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania
imepiga hatua katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia vifo
54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000 Aidha,
mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania
imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa
polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.
“Ninaeleza kwa masikitiko
kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini Tanzania
ambapo hadi kufikia tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia 21,581,kati
yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia wizara ya afya
itaimarisha na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira katika kukabiliana na
ugonjwa huu”
alisema Kwa upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania
imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa
Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa
hadi kufikia asilimia 0.6 .
Katika kuboresha huduma za afya nchini alisema Serikali ya
Tanzania imejipanga na kuhakikisha itaboresha huduma za afya ziweze kumfikia
kila mtanzania popote alipo, “ili kuweza kufikia malengo haya ni wakati muhimu
sasa kuwekeza zaidi katika sekta hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali
fedha,watu pamoja na kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya
nchini”.
Waziri Ummy alisema katika kufikia mafanikio ,wizara ya afya
inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016
wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa
kwa mwananchi katika kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha
au kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.
Mkutano mkuu wa mwaka wa Afya Duniani hufanyika nchini Geneva
–Uswis kila mwaka mwezi mei ambao huwakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi
wanachama wa Shirika la afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau,mashirika na
taasisi zinazoshiriki katika kutoa huduma za afya Duniani.
Tanzania inawakilishwa na waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy
mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo.
![]() |
Waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu
kushoto akiwa na waziri wa
afya Zanzibar Mhe.Mahmoud
Kombo wakifuatilia madazinazowasilishwa kwenye
mkutano
huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama
wa shirika
la afya duniani(WHO),nyuma yao ni katibu mkuu wizara
ya afya Tanzania bara dkt.Mpoki Ulisubisya.
![]()
Waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu
kushoto akiwa na waziri wa
afya Zanzibar
Mhe.Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa
kwenye
mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa
afya kutoka nchi wanachamawa shirika
la afya duniani
(WHO),nyuma yao ni katibu mkuu wizara ya afya
Tanzania bara
dkt.Mpoki Ulisubisya.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni