Msanii Nyota Ndogo ameingia katika mgogoro na familia yake
baada ya kuamua kufunga ndoa na mpenzi wake ambae ni mzungu raia wa Denmark, Mgogoro huo umewekwa bayana na kaka yake Nyota Ndogo anaejulikana
kwa jina la Juma Tutu, jana tarehe 22 katika mitandano ya kijamii instagram na facebook nyota ndogo alitupia picha za tukio la ndoa yake huku akielezea hisia kutokana na furaha aliyokua nayo,
Akizungumza na Redio Citizen iliyopo nchini Kenya leo hii kaka
yake Nyota Ndogo Bw. Juma Tutu amesema kua mgogoro huo ulizuka baada mzungu huyo kukataa
kulipa mahari kama ilivyo ada na desturi za kiafrika mwanamke hulipiwa mahari na
ndipo taratibu za kufunga ndoa hufanyika,
Katika mahojiano na kituo cha Citizen Radio kaka yake Nyota
ndogo alisema yafuatayo
“Sijui kama kuna harusi ya kiafrika ambayo inafanywa
bila mahari, na hivi ninavokuelezea na mama yangu mwenyewe hakwenda harusi niko
nae mimi hapa alikataa kwenda harusini sababu kubwa ya mama kukataa kwenda
harusini ni yule mzungu.. yule kibabu alikataa kabisa kutoa mahari.
maana
tulimuita akakwepa kwa madai kua alikua anaenda ulaya lakini Nyota Ndogo akampigia magoti akisema oooh
nioe basi bila mahari, sasa mimi kwa upande wangu niliona dada yangu kwa upande
wa musiki ni international musician super star
yawezekana wanaume wanampigania yeye sasa inakuaje tena yeye anamlilia
yule mzungu mzee akifikiri kwamba yule mzungu ana hela,
basi mimi nikachukizwa
sana na kitendo hicho, Nyota ndogo haambiliki hamzikizi mtu yeyotee yule babu
wala nyanya wala nani akisha amua lake kasha amua ni kama ule mti wa mlelema alivosema mzee ngala mti ameshindwa nyani kupanda ndio yeye basi,
mimi bifu yangu kwenye mtandao wa
kijamii kuna watu ambao hawanielewi kuna post ile niliiweka, nyota ndogo
anaishi maisha ya dhiki sio ile maisha ya kuonekana kwenye tv, magazeti sijui
wapi anasafiri maisha ya nyota ndogo ni mbaya sana hana kitu mama yake
anateseka kabisa nilikua mimi na mama karibu siku tatu nimemwambia nyota ndogo
aje tuzungumze tuyatatue haya maneno alikua anasema hajali chochote wala hajali
mama wala mimi aidha twende harusini ama tusiende potelea mbali haambiliki keshakua
star yeye anajua kila kitu duniani” hayo ndio maneno ya Juma Tutu kaka yake Nyota ndogo
Wakati kaka yake akizungumza hayo Nyota Ndogo ameonekana
kuto jali hali ya sintofahamu iliyopo baina yake na familia yake na kwamba
amezama katika mahaba ya M Denmark huyo na badala yake amekua akiandika post katika
ukurasa wake wa facebook kuelezea hisia zake juu ya furaha aliyonayo baada ya kufunga
ndoa na mwandani wake huyo mzungu,
baadhi ya post zake katika mtandao wa kijamii wa facebook Nyota Ndogo ameandika maneno yafuatayo
“kweli mapenzi bahari
Nikaha ilikuwa ya kufana Henning Hussein Nielsen Ndoa Ni
wamuzi wa dhati toka moyoni na Nafsini. Ukipenda
hunabudi kujitosa kwenye dimbwi la mapenzi.naahidi nitakuwa mke wako siku zote.
I will
always be with you forever ever.inshallah Mola atuongoze atujalie Amina.
Mashallah
#mtotowakikesimama” huo ndio ujumbe wake huku ukichombezwa na picha hiyo hapo chini

Siku kuu katika maisha yangu ni leo
nimejawa na furaha tele
ndoa ni safari ndefu na inahitaji moyo. Nawatakieni muniombea dua zenu
inshallah..Huyu ndo chaguo langu.
To
love and be loved is to feel the sun from both sides.
I love my husband Henning Nielsen” huu ni ujumbe wa pili ukachombezwa kwa picha hizo hapo chini


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni