Alhamisi, 12 Mei 2016

Walimu walipwa Vifaranga vya kuku kama malipo ya mshahara baada ya serikali kukumbwa na ukata


Wakati nchini Tanzania walimu wakiomba kuongezewa mishahara, Mji mmoja nchini Uzbekistan umekua ukiwapa waalimu wake kuku kama mshahara badala ya pesa

Mamlaka za mji wa Nukus katika jimbo linalojitawala la Karakalpakstan wamekua wakiwalipa vifaranga wachanga kwa walimu kutokana na uhaba wa pesa nchini humo.

Kituo cha radio kinachofadhiliwa na Marekani (Radio Ozodlik) kimemnukuu mwalimu mmoja akilaani hatua hiyo kama aibu kubwa kwa mamlaka.

Mwalimu huyo aliyeghadhabishwa na hatua hiyo amesema hataki vifaranga kwa sababu anaweza kuwapata sokoni, lakini wanataka pesa zao.

Vifaranga wanaotolewa kama mshahara wana gharama ya dola mbili kila mmoja, ikiwa ni maradufu bei inayouzwa vifaranga sokoni.

Uzbekistan imekumbwa na uhaba wa fedha kwa miaka sasa hali inayosababisha serikali kuchelewesha mishahara ya wafanyikazi na malipo ya uzeeni.

Mapema mwezi huu wafanyikazi wa serikali katika mji mkuu,Tashkent walilalamikia kwamba hawakuwa wamelipwa mshahara kwa miezi miwili kwa sababu benki hazikuwa na pesa
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni