Jumatatu, 16 Mei 2016

Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba, amewaahidi wakulima kutatua migogoro ya Ardhi


Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba jana amekutana na wafugaji,wavuvi na wakulima zaidi ya 400 kutoka kanda mbalimbali za nchini.

Katika mkutano wake na makundi hayo uliofanyika mapema asubuhi hii Ukumbi wa LAPF-Dodoma,Mwigulu amesikiliza kero za wafugaji,wavuvi na wakulima kwa vielelezo vya maeneo yenye matatizo,na suluhisho lake.Kero hizo kupitia vielelezo mbalimbali ziliwasilishwa kwa Mwigulu katika kikao hicho kwa kila kanda kupitia uongozi husika wa makundi hayo,moja tatizo kubwa ni matumizi bora ya ardhi na umiliki wake.

Akizungumza na makundi hayo,Waziri Nchemba amesema "hatua ya kwanza ya kupambana na tatizo la ardhi ambalo ni kubwa kati yetu,wizara yangu kwa kushirikiana nanyi kupitia ripoti hizi tunafanya ubainisho wa kila eneo lenye mgogoro kujua umiliki wake,uhitaji wake na matumizi yake kama yamepitwa na wakati au bado eneo hilo linahitajika.

 "Kuna maeneo yanayomilikiwa na watu wa maliasili,tunafanya nao kazi kwa karibu kubainisha mapori ambayo yameshapoteza sifa zaendelea kuhifadhiwa iliyagawiwe kwa utaratibu kwa wafugaji wetu na wakulima.Lakini ni wajibu wa kila mfugaji kwa serikali hii kuachana na ufugaji holela,ufugaji wa ng'ombe wengi wasio na tija.

Tumedhamilia kufuga kwa kisasa kupitia vitalu 'Blocks",tulishatenga maeneo na kuwagawia wafugaji itakuwa ni njia sahihi kuelekea uwekezaji wa viwanda vingi vya nyama,maziwa n.k kwasababu tutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa ng"ombe wa kisasa kwenye hivyo vitalu.

" Vilevile waziri Nchemba amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia kauli na dira ya Rais wetu,wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi imejipanga kutatua kero mbalimbali za sekta hii.

Kwa sasa mbali ya ripoti za wakulima,wafugaji na wavuvi walizoziwasilisha wizarani kuhusu kero hizo,kuna wataalam kutoka wizarani na mikoani wanazunguka kila eneo linalotakiwa kufanyiwa kazi kwaajili ya kuondoa migogoro na kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi hiyo.

Wizara yake inashirikiana na Wizara ya ardhi,wizara ya maliasili na wizara zingine kuhakikisha migogoro ya ardhi na malisho inabaki historia katika Taifa letu





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni