Jumatatu, 20 Juni 2016

Baada ya kuzagaa kwa taarifa za kuibiwa kwa KIFARU cha JWTZ, Jeshi hilo limelitaka Gazeti lililo andika habari hiyo kuomba radhi!


Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Ngemela Lubinga amekanusha vikali  taarifa za kuibiwa kwa kifaru na kusema kuwa hazina ukweli.


Lubinga amesisitiza kuwa, JWTZ ni jeshi ambalo lipo imara  katika ulinzi kwa maeneo yote ya nchi hivyo ni aibu na fedheha kubwa kwa Gazeti kutoa habari za kupotosha hali ambayo inaleta picha mbaya kwa jeshi ambalo limekomboa nchi nyingi za afrika na kulinda amani duniani .

Hata hivyo amesema kua jeshi hilo lipo imara na ni jeshi ambalo linamafunzo thabiti hivyo ni jambo ambalo haiingii akilini kwa mtu makini jeshi kuibiwa Kifaru.

Aidha aliongeza kua makini wa jeshi huanzia awali katika usaili wakati wa kuajiri kwani kumekuwa na mchujo kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa sanjari na kupita mafunzo ya JKT.
Hata hivyo amelitaka Gazeti lililoandika habari hizo liombe radhi kwa taarifa yake hiyo.


Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Ngemela Lubinga.

Mapema leo Juni 20.2016 kumeibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii juu ya gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki kuandika habari juu ya kuibiwa kwa kifaru cha jeshi, huku watu/wananchi wakiipokea kwa hisia tofauti za kuibiwa huko.


Baadhi ya maadishi katika gazeti hilo yalisomeka kama ambavyo kipande cha gazeti hilo kinavyo onekana na kusomeka hapo chini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni