Wabunge wa Vyama vya
Upinzani vinavyounda Ukawa, kwa mara nyingine tena leo wametoka Bungeni kama
walivyoazimia kususia vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia
Ackson.
Tofauti na siku nyingine, leo wabunge hao wametumia mtindo au style ya
aina yake ambapo waliiziba midomo kwa kutumia karatasi na plasta huku akiandika
jumbe tofauti tofauti kuashiria kunyimwa uhuru na haki ya kidemokrasia ya
kujieleza.
Akielezea sababu za kuto shiriki mkutano wa Bunge na kutoka nje Mwenyekiti
mwenza wa Ukawa Mh. James Mbatia amesema kua kwakuwa leo ni siku ya kupiga kura
hivyo wao wameamua kuto shiriki zoezi hilo kwa kuwa hawakushiriki kujadili
bajeti hiyo na kuongeza kuwa bajeti hiyo inamkandamiza mtanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni