Jumatatu, 13 Juni 2016

Kijana wa miaka 29 ashambulia Club ya mashoga na kuua 50, na kujeruhi wengine 53


Watu 50 wauawa baada ya mtu mmoja kushambulia klabu ya mashoga nchini Marekani

Raia wa Marekani, Omar Mateen 29, ameishambulia kwa bunduki klabu ya mashoga iliyopo Orlando nchini Marekani.

Mateen, anayetokea ambae ni mkazi wa Florida, ameua takriban watu 50 na kujeruhi wengine 53 na kuwashikilia mateka.

Polisi walitumia mabomu kumchanganya mtu huyo na kuwaokoa watu karibu 30 waliokuwa wamewashikilia mateka. Mateen alipigwa risasi na polisi saa kumi na moja alfajiri baada ya tukio hilo kudumu kwa masaa matatu.

Hilo ni tukio baya zaidi la aina hiyo kuwahi kutokea Marekani. Maofisa kwenye hospitali ya Orlando wamedai vifo vinaweza kuongeza.  Muda mfupi kabla ya shambulio hilo, Mateen alipiga simu 911 kuelezea utii kwa kundi la ISIS.

Baba yake Mateen, akiongea na NBC News amesema kuwa mwanae amekua akiwachukia mashoga na alianza kuwachukia baada ya kuwaona wanaume wawili wakipigana busu huko Miami miezi kadhaa iliyopita jambo hilo lilionesha kumkera sana Mateen.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni