Ellertoni Mwamasika (Mkurugenzi wa Chuo cha Ilemi PolyTechnic) |
Baraza
la Udhibiti wa Vyuo vya Ufundi nchini Tanzania NACTE imekifungia chuo cha
Biashara, Mifugo na Kilimo cha Ilemi Polytechnic kilichopo Mkoani mbeya kwa kushindwa kukidhi vigezo
ikiwa ni pamoja na kudahili wanafunzi wasio na sifa.
Akisoma
uamuzi huo kwa niaba ya NACTE, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla amesema kuwa
taarifa kutoka NACTE zinaonesha kuwa chuo kina mapungufu mengi ikiwa ni
pamoja na kutoa mafunzo ya mifugo ambayo hayajathibitishwa na vyombo husika vya
serikali.
Pia
amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikidahili wanafunzi wasiokuwa na vigezo,
akitolea mfano wanafunzi wanaosoma kozi ya mifugo ambapo kati ya wanafunzi 359
ni wanafunzi 89 pekee ndiyo wanaotambulika kuwa na vigezo husika.
Wakizungumza
kwa uchungu baadhi ya wanafunzi wamelalamikia chuo hicho kwa kuwasababishia
upotevu wa muda na gharama, ambapo baadhi yao walikuwa tayari wamehitimu na
walikwenda chuoni hapo kufuatilia vyeti.
Nae Catherine Buda ambae ni muhitimu wa chuo hicho akitoa lawama kwa uongozi wa huo hicho alisema haya "amesema kua Mimi
nimetoka mbali, nimekuja kufuatilia cheti changu, sasa nina miezi miwili hapa,
kila siku nazungushwa nazungushwa, kumbe walijua wanakuja kufungiwa, kwa hiyo
cheti changu sipati, na muda nimepoteza, nimekaa hapa miaka mitatu halafu leo
naambiwa miaka yangu mitatu haina maana tena, sikubali sikubali..”
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Ellertoni Mwamasika, ameomba radhi na
kusema kazi ya kuendesha chuo ni ngumu “Chuo
kinawaomba radhi wote, ila mjue kuwa kazi hii ya kuendesha chuo ni ngumu”
Hata hivyo serikali imesema wanafunzi wenye sifa watahamishiwa katika vyuo vingine huku ikimuagiza mmiliki wa chuo hicho kuwalipa wanafunzi gharama zao zote kabla hawajatoka chuoni hapo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni