Mkesha umefanyika huko Orlando mjini
Florida pamoja na maeneo tofauti duniani ili kuwakumbuka waathiriwa wa
shambulio katika kilabu moja ya usiku ya wapenzi wa jinsia moja.
Kiongozi
mmoja wa kiislamu aliwaambia wale wanaohudhuria mkesha huo kwamba
Waislamu wanaungana nao kupinga chuki ,mauaji na uharibifu.
Mikutano kama hiyo pia ilifanyika katika mataifa kama vile Ufaransa,Australia Uingereza na Ujerumani.
Shambulio hilo la kilabu ya usiku lilisababisha mauaji ya watu 49 huku makumi wakijeruhiwa
Mamlaka nchini Marekani inasema kuwa mshambuliaji Omar Mateen aliahidi utiifu kwa kundi la wapiganaji wa Islamic State muda mfupi kabla ya shambulio hilo.
Wateja kadhaa wa Pulse wameviambia vyombo
vya habari nchini Marekani kwamba Mateen alikuwa akiingia katika kilabu
hiyo mara kwa mara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni