Imani Kajura Mkurugenzi Eag Group, muwezeshaji katika Kongamano la Wanavyuo lililofanyika Mbeya siku ya Jumamosi. |
Wanafunzi wa vyuo nchini washauriwa kuunda vikundi mbali mbali vya
ujasiliamali kisha kuiomba serikali kuviwezesha ili kujitengenezea kipato.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa Eag Group ndugu Imani Kajura
wakati akizungumza na wanavyuo walio hudhuria katika chakula cha jioni (dinner)
jijini Mbeya baada ya Kongamano la wanavyuo lililo andaliwa na Mzumbe Campus ya
Mbeya ambalo lilifanyika mchana tarehe 11/6/2016 siku ya jumamosi.
Kajura alisema sasa hivi serikali imeahidi kutoa kiasi cha
shilingi milioni hamsini kwa kila kijiji hivyo wanavyuo wangeweza kutumia fursa
hiyo kuunda vikundi kisa kuiomba serikali kuvitazama vikundi hivyo kama kijiji na
hatimae kuviwezesha kwa kuvipatia mikopo hatimae kuitumia kama mtaji wa kuwawezesha kufanya shughuli za uzalishaji uchumi ili kujikwamua.
Aidha alisema suala la wanavyuo nchini kutegemea mikopo pekee si
jambo jema kwani wamekua wakitumia muda mwingi kufuatilia mikopo na hali hua
mbaya zaidi pindi mikopo hiyo inapochelewa kwani hulazimika kuandamana na
kufanya fujo jambo linalopelekea baadhi yao kupoteza muda wa masomo na hata kufukuzwa kabisa chuo kutokana na kutofuata sheria na kanuni za kudai haki ya mikopo hiyo.
Asema kama wanavyuo wakiamua kuunda vikundi na kuishawishi
serikali kuwapa mikopo itawezekana kwa kua wanafunzi hawa hutambulika kisheria
lakini pia si rahisi kikundi chote kutoroka na kushindwa kulipa mikopo hiyo
kwani wanafunzi hawa hufaamiana vyema hivyo ni rahisi kuunda vikundi
kulingana na matakwa yao.
Imani Kajura alilazimika kutoa ushauri huo baada ya Mwanasheria wa
Mahakama Kuu na Mjasiliamali ndugu Albert Msando kutoa maoni kwa niaba ya
wanavyuo
Akiwasilisha maoni hayo kwa mgeni rasmi Mhe. Luhanga Mpina ambae ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Msando alisema kwanini serikali isiandae mpango/mkakati
maalumu wa kuwawezesha wanavyuo walio hitimu kwani wanavyuo wengi wamekua
wakihaha mtaani kwa kukosa hata mitaji ambayo ingeweza kuwasaidia hata
kuanzisha biashara kwani matarajio ya
wanavyuo wengi ni kujiajiri na kuajiriwa na ajira hizi hupatikana mijini zaidi
hivyo baada ya wanafunzi kuhitimu hulazimika kurudi nyumbani kwa wazazi kwa
ajili ya kusubiria vyeti kwa kua hawana uwezo wa kuendelea kubaki mjini na
kujishuhulisha na chochote,
Msando aliendelea kusema kua wanavyuo wengi hushindwa kuanza
maisha kwa kua baada ya kumaliza vyuo wanakosa kitu ambacho kinaweza kua ni
dhamana ya wao kuweza kukopa hasa katika benk na vikundi mbali mbali vya mikopo.
Hata hivyo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira Mhe. Luhanga Mpina akitoa ufafanuzi kuhusina na ushauri uliotolewa
alikiri kuupokea ushauri huo na kuufikisha serikalini ili uweze kufanyiwa kazi.
“Kwa kuwa serikali tuliyonayo ni makini
nawahakikishieni kua ushauri huu nimeuchukua na nitaufikisha serikalini ili
kuona namna ambavyo serikali inaweza kuandaa utaratibu wa kuwasaidia wanavyuo
walio hitimu” alisema Mpina
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Luhanga Mpina akitoa ufafanuzi kuhusina na ushauri uliotolewa |
Picha ya pamoja ya wanavyuo waliojitokeza kuelezea namna walivyo nufaika na kongamano hilo na wataitumia vipi elimu hiyo. . |
Picha ya pamoja Wawezeshaji na wanavyuo ambao walijishindia zawadi ya simu aina ya Huawei baada ya kueleza wamenufaika vipi na kongamano la wanavyuo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni