Polisi Kahama
wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya makundi ya wananchi waliokua
wamekusanyika katika maeneo mbali mbali kwa wakijiandaa kuhudhuria mkutano wa
Chadema.
Mabomu hayo
yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya wananchi hao
waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara ulio kua umepangwa kufanyika leo kuanzia saa 9:00 alasiri kabla ya polisi kupiga
marufuku mikutano na maandamano ya aina yoyote ya kisiasa nchini
Jeshi la polisi
leo jioni lilitoa taarifa ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa ambapo katika taarifa hiyo jeshi la polisi limesema sababu za kupiga
marufuku mikitano na maandamano hayo ni kufuatia uchunguzi wake uliofanywa kupitia vyanzo mbalimbali ambao ulibaini mikutano hiyo ina nia ovu yenye lengo la kuwashinikiza wananchi kuto tii sheria pamoja na
kuvuruga amani
Hata hvyo katika
taarifa hiyo jeshi la polisi limesema kuwa halitasita kuchukua hatua kali za
kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni