Eric Aniva amekamatwa kufuatia agizo la Rais Peter Mutharika
kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya rais Bright Molande.
Amesema kuwa Bw. Aniva aliyepewa jina la utani kuwa 'fisi' kwa
jukumu lake katika uovu huo atashtakiwa kwa kukiuka haki za watoto.
Inaelezwa kuwa rais Mutharika amechukizwa na taarifa hiyo
na ameapa kukabiliana na tamaduni hiyo.
Mtu
aliyetajwa katika habari hiyo ambaye alifanya mapenzi na zaidi ya wasichana 100
pia imebainika kuwa alikuwa na virusi vya ugonjwa wa ukimwi.
Tamaduni hiyo ya usafishaji ilipendekezwa na kufadhiliwa na
baadhi ya jamii kusini mwa Malawi lakini serikali imejaribu kuisitisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni