Dkt. Charles Tizeba akiapishwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi June 13 mwaka huu, Ikulu Jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi, Dr.
Charles JohnTizeba ametangaza kuwa ofisi yake itahamia Dodoma wiki ijayo.
Uamuzi huo umekuja baada ya
Waziri
Mkuu kutangaza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Mashujaa kwamba ofisi
yake itahamia Dodoma ifikapo Septemba na wizara nyingine zitamfuata.
Waziri Tizeba alisema hayo jana baada
ya kukutana na wadau wa mifuko ya hifadhi ya jamii na bandari kujadili
uwekezaji katika uvuvi wa bahari kuu ili serikali iweze kuongeza pato la Taifa
kupitia sekta hiyo.
Agizo la ofisi za serikali kuhamia Dodoma lilitolewa
na Rais Magufuli siku ya Mashujaa hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni