Ijumaa, 29 Julai 2016

DKT. KIGWANGALLA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA VIONGOZI WA MFUKO WA ABBOTT (ABBOTT FUND) KUTOKA MAREKANI.


Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Ujumbe  wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake hapo jana.
Makamu wa Rais wa  Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania Andy Wilson akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani na Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam jana kuzungumzia masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) jana jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelewa na  ujumbe  wa viongozi wa mfuko huo kutoka nchini Marekani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni