|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Said Mohamed mkazi wa Mafia ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Mkazi huyo wa Mafia alimueleza Makamu wa Rais juu ya ugumu wa upatikanaji wa Dawa.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa serikali itanunua mashine mbili za kisasa za
mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zitasaidia kwa
kiasi kikubwa utoaji
wa matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu katika
Taasisi hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassan ametoa ahadi hiyo
wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara fupi ya
kutembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na Kumtembelea na kumpa
pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye
anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa
hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili
wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.Kuhusu
uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali
itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Baadhi
ya wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi ya Saratani
ya Ocean Road na wameomba serikali iendelee kuipatia taasisi hiyo vifaa vya
kisasa vya kutolea tiba kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa
wanaokwenda kupata matibabu ya saratani.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi (katikati) ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Bi. Maria Maliseli Boniface wa Kilosa Morogoro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Calist P. Mushi mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo (kulia) wakati wa kutembelea Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na wananchi waliokuja kuwaona ndugu na jamaa zao ambao wamelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Wananchi hao walimueleza Makamu wa Rais haja ya kuongezwa kwa mashine za mionzi suala ambalo Makamu wa Rais aliwajibu kuwa zitafungwa mashine mpya mbili katika mwaka huu wa fedha 2016-2017 ilikurahisisha matibabu. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni