Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira NEMC limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha
kutengeneza simenti cha Dagonte Industry limited kilichopo mjini Mtwara kusini mwa Tanzania,
kwa kosa la
kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Katika siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara
Imebainika kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu
kianze kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa
sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na utaratibu
mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani hapo, kukosa vyoo
kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva na makondakta wanao
chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali
za nchi, pamoja na kutokusakafia sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo
imeelezwa kuwa eneo hilo la nje wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake
huatarisha afya ya watumiaji wa eneo hilo.
Kwa Mujibu wa Naibu
waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote inayotakiwa kulipwa ndani ya
wiki mbili, inaenda sambamba na urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo
pamoja na kuhamsha uongozi wa kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira,
na kutaka kiwanda hicho kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.
Kwa upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho
Bw. James Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa
kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya hivyo
kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa baadhi ya
miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa baadhi ya vibali
kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria ya mazingira.
Naibu waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza
gas cha Madiba na kukisifu kwa
utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya serikali, kuwa
mfano katika kutii sheria za mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni