Bw. Eric Aniva (40) akionesha mzizi ambao anautumia kumwoshea binti kuondoa mikosi baada ya kumbikiri. |
Wakati nchini Tanzania na baadhi ya nchi za kiafrika wakionesha
kuthamini kitendo cha mwanamke kukutwa akiwa kautunza usichana wake (bikra)
pindi anapo olewa kwa kua jambo hilo hudhihirisha mwanamke huyo amelelewa na
kutunzwa vema hali imekuwa tofauti katika
jamii moja nchini Malawi ambapo haithamini
ubikira wa mtoto wa kike.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wolrec umeeleza kuwa nchini Malawi pindi
binti anapovunja ungo na kuona hedhi yake ya kwanza wazazi wa binti huyo
hulazimika kumtafuta mwanaume maarufu kama fisi na kumlipa kiasi cha fedha kwa ajili ya kumbikiri
binti yao ili kuondoa mikosi, wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo
mengi ya kusini mwa Malawi huamini kuwa binti kuendelea kukaa na bikra baada ya
kuvunja ungo husababisa mikosi katika jamii.
Kwa mujibu wa tafiti zilizo fanywa na kutolewa na mtandao wa
Wolrec matukio hayo yamekuwa yakifanywa zaidi katika Wilaya za Lilongwe na
Blantyre nchini humo na miongozi mwa wanaume maarufu na maalumu kwa kazi ya
kubikiri kisha kujipatia ujira ni bwana Eric Aniva mwenye umri wa miaka 40
mkazi wa kijiji cha Nsanje amekiri kuwa tangu aanze kazi hiyo amesha wabikiri
washichana zaidi ya 100, ambapo wazazi ndio hubeba jukumu la kuwachaguliwa
mabinti zao mwanaume wa kuwaondolea mikosi kwa kumbikiri.
Aniva ambae ni baba wa watoto 5 na wake 2 amesema kuwa katika
jamii yao huamini kuwa iwapo mwanamke au binti atakataa asibikiriwe baada ya
kuvunja ungo na kuona hedhi yake ya kwanza basi ndugu wa huyo binti watakuwa
wakikabiriwa na mikosi pamoja na magonjwa.
Aniva anafafanua zaidi kuwa pindi anaposhiriki ngono wa watoto
hao wenye umri kati ya miaka 11-14 huwa anapewa siku 3 kwa ajili ya kumsafisha
na kumuondolea mikosi na kwamba maandilizi ya binti kubikiriwa hutanguliwa na
sherehe kubwa ambapo binti hupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi zake na
baada ya hapo hupelekwa kubikiriwa.
Aidha anasema kabla ya kuanza kumbikiri msichana alievunja ungo
hulazimika kufanya maandalizi ya kuchemsha mizizi au dawa kwa siku tatu na
kubainisha kila anapombikiri binti hulipwa kiasi cha dola $7.
Hata hivyo Aniva amesema kuwa si mabinti pekeee ambao yeye
hufanya nao ngono na kuwabikiri ili kuondoa mikosi bali hata mwanamke aliefiwa
na mumewe hulazimika kufanya nae ngono kabla ya kumzika mumewe ili kuondoa
mikosi sambamba na wanawake
walioharibikiwa mimba nao pia hulazimika kufanya hivo ili kuondoa mikosi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni