Taarifa
inatolewa kwa vyombo vya habari kwamba Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), itakutana kwa dharura, jijini Dar es Salaam, chini ya
Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, ambapo pamoja na masuala mengine,
itapokea taarifa na kujadili hali ya siasa nchini.
Katika
siku za hivi karibuni, taifa limekuwa likipitia katika majaribu makubwa, ikiwa
ni pamoja na uvunjifu mkubwa wa sheria na taratibu za kuongoza nchi unaofanywa
waziwazi na mamlaka za juu/viongozi waandamizi wa nchi kupitia kauli na matendo
mbalimbali kiasi cha kuwashtua Watanzania ambao wangependa kuona nchi yao
ikiendeshwa katika misingi ya uwajibikaji wa kisheria na demokrasia.
Katika
kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24, mwaka huu, Kamati Kuu pia itapokea
taarifa na kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu mipango mbalimbali
inayoendelea ya kukipanga chama ili kiendelee kufanya shughuli zake kwa ufanisi
hususani kinapokwenda kuimarisha misingi kuanzia ngazi ya kitongoji nchi nzima,
kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.
Imetolewa
leo Ijumaa, Julai 22, 2016 na;
Tumaini Makene-Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na
Habari
CHADEMA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni