Jumatatu, 18 Julai 2016

Mtalii kutoka Afrika ya Kusini, afia mlima Kilimanjaro!!

Guguleth Mathebula Zulu 38
Raia wa Afrika ya kusini, Guguleth Mathebula Zulu mwenye umri wa miaka 38 amefariki dunia leo baada ya
kupatwa na tatizo la kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa mlima wa mlima wa Kilimanjaro.

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanapa) Paschal Shelutete amesema shirika hilo kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali zinaendelea na uratibu wa kurejesha mwili wa marehemu Afrika ya Kusini kwa mazishi.

Shelutetea amesema Zulu alifika nchini na kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro Julai 14 kuenzi jitihada za Rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela za kusaidia familia masikini nchini Afrika ya Kusini, hususani kuwapatia mahitaji muhimu watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji hayo.

Hii ni mara ya pili kwa watalii kutoka Afrika ya Kusini kupanda  Mlima Kilimanjaro kuenzi juhudi za Mandela katika ikiwa ni jitihada za kusaidia watoto wa kike.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni