Jumamosi, 16 Julai 2016

Serikali yasema inatambua mchango wa hospitali za mashirika ya dini hapa nchini

Na.Catherine Sungura,Muleba


waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kagera,wilaya ya Muleba,Wamiliki wa hospitali teule ya Rubya pamoja na watumishi wa hospitali hiyo 


Serikali inatambua na kuthamini mchango
wa hospitali za mashirika ya dini katika kutatua matatizo ya wananchi nchini.

Hayo yamesema jana na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea hospitali teule ya wilaya ya Rubya iliyopo wilayani Muleba

"Sera ya afya ni ileile hivyo tutaendelea kushirikiana katika kuboresha huduma zinazotolewa na madhebebu ya dini,hivyo bado ipo haja ya kufanya kazi nanyi"alisema

Waziri ummy alisema licha ya changamoto kubwa ya watumishi,wizara yake itaendelea kuwapangia watumishi katika hospitali hizo bila kudhoofisha utendaji wao

Alisema upungufu wa watumishi katika sekta ya afya nchini ni asilimia 48 ila kwa mkoa wa kagera upungufu ni asilimia 54,hivyo mkoa una uhaba mkubwa wa watumishi katika sekta ya afya.

Aidha,amesisitiza hospitali hizo kufuata taratibu za kiutumishi kwa kutoa taarifa sahihi za kuajiri mbadala wa watumishi wastaafu na wale wanaofariki ili kuondoa watumishi hewa na wale wasiokuwa na sifa kwa kulipwa malipo yasiyo halali.

"Hatutamlipa mtumishi mshahara kwa keshi kwa watumishi wote waliopo kwenye hospitali teule zinazomilikiwa na mashirika ya dini bali tunahitaji watumishi wote walipe kupitia akaunti zao za bank ili kuondoa tatizo lililopo hivi sasa

Mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa yenye hospitali nyingi zinazomilikiwa na mashirika ya dini nchini ambapo kati ya hospitali 14 za  mkoa huo, serikali ina miliki hospitali mbili tu.

Waziri wa afya akisalimiana na viongozi wa madhehebu ya kidini zinazomiliki  hospitali katika mkoa wa Kagera.


Waziri Ummy akimjulia hali mama aliyejifungua katika wodi ya wazazi kwenye hospitali teule ya Rubyas.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni