Ijumaa, 8 Julai 2016

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini Kenya ajinyonga baada pesa yake kuliwa aliyoweka katika utabiri wa mchezo wa Mechi za Euro 2016

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu nchini Kenya hivi karibuni amejiua kwa kujinyonga baada ya kupoteza dau la shilingi 80,000 sawa na dola $800 aliloweka katika mechi za Euro 2016.
Kwa mujibu wa gazeti moja nchini Daily Nation mwanafunzi huyo alikuwa ameweka dau la dola $ 400 kwa ushindi wa Ujerumani na pesa zingine sawa na hizo kwa ushindi wa Italia.
Hata hivyo kinyume na matarajio yake mechi hiyo iliishia sare na kumaanisha kuwa alikuwa amepoteza pesa hizo zote.
kufuatia matokeo kuwa tofauti na kile alichotaraji, mwanafunzi huyo alifunga safari kutoka mjini Nairobi hadi kwao magharibi mwa Kenya katika kijiji cha Ondome Uriri jimbo la Nyanza ambapo alijitia kitanzi nyuma ya nyumba ya mamake mzazi.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo David Kirui anasema kuwa marehemu aliacha ujumbe akisema hakuona haja ya kuendelea kuishi baada ya kupoteza pesa alizopewa za kulipia karo za chuo kikuu.
Ujerumani hata hivyo ilishinda kwa mikwaju ya penati iliyo.
swala la kuenea kwa michezo ya bahati na sibu nchini Kenya limezua  mjadala kwa baadhi ya wapenzi wa kandanda na jamii kwa jumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni