Ijumaa, 8 Julai 2016

Waziri Mwigulu Nchemba amtembelea Askari aliyejeruhiwa wakati akipambana na majambazi katika tukio la uporaji Benki ya Access!!

Mh.Mwigulu Nchemba akiwa nyumbani kwa askari PC.Shaban

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Nchemba amemtembelea askari PC.Shaban nyumbani kwake Temeke ili kumjulia hali.

Askari F.9060.PC.SHABAN alijeruhiwa wakati wa mapambano na majambazi akiwa kazini(lindo) kwenye BENKI ya ACCESS tawi la Mbagala, ambapo katika tukio hilo la ujambazi lilipelekea kupoteza maisha kwa askari mmoja na kujeruhi wafanyakazi wa Benki hiyo.



Mnamo February 26. 2016 Majambazi ambao idadi yao haikufahamika wakiwa na mabomu na bunduki za kisasa walivamia Benki ya Access, Tawi la Mbagala wakapora viroba vya fedha, na kumuua askari mmoja na baadae wanne kati yao wakauawa na polisi.

Majambazi hao walidaiwa kufika katika benki hiyo kwa bodaboda nne majira ya saa nane mchana na kufanya mauaji kisha kubomoa kwa risasi mlango wa vioo na kuingia ndani na kuzua hataruki kubwa katika tukio hilo ambalo lilidumu kwa karibu saa moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni