Watu
zaidi ya mia tatu nchini wamefanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa vikope(Trakoma)
kutokana na serikali kuweka mikakati ya kuyatokomeza na kuyaondoa kabisa.
Hayo yamesemwa leo na mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu dkt. Mwele Malecela wilayani mnduli wakati wa zoezi la uhamasishaji wa umezaji dawa za kuzuia trakoma na upasuaji wa ugonjwa huo.
Dkt. Malecela amesema zoezi hili ambalo ni endelevu kwa wilaya zilizoathirika na ugonjwa huu inasaidia kumaliza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Aidha wananchi
wanatakiwa kuhakikisha wanakunywa dawa, kufanyiwa upasuaji pamoja ya kuwa safi
wao pamoja na mazingira wanayoishi.
Baadhi ya wakazi wa kijijo hicho wakisubiri kupatiwa kingatiba ya ugonjwa wa trakoma (Picha zote na Catherine sungura - wizara ya afya). |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni