Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Zakaria Benjamin mwenye umri wa
miaka 35, mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma za kuingia na kujifanya daktari katika Hospitali ya rufaa mkoa wa
Morogoro wakati hana taaluma hiyo.
Daktari huyo feki anadaiwa aliingia katika hospitali hiyo ya rufaa
Julai 10 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri huku akijifanya kukagua na
kutembelea wagonjwa katika wodi mbali mbali hospitalini hapo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema daktari
huyo alitembelea wodi namba 1,7 na 9 na
kujifanya kuwa yeye ni daktari mgeni hivyo anakagua wagonjwa kuona kama
wamepata huduma ipasavyo.
Mtuhumiwa huyo alipofika katika wodi namba 7 alienda katika chumba
cha kubadilisha nguo kisha kuvalia koti la kidaktari lililokuwa limeegeshwa
mahali hapo.
Kamanda Matei amesema mtuhumiwa huyo aliingia hospitalini hapo
isivyo kihalali kwa lengo la kutaka kuiba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni