Haki hizi
zinatoka katika Sura ya 20, Sheria
ya Mwenendo wa Makosa ya jinai
kifungu cha 48 hadi 59. Ni haki
ulizonazo ikiwa utazuiliwa na kuhojiwa na polisi.
1. Ni
lazima polisi akutajie jina lake pamoja
na cheo chake kabla hajakuhoji.
2.
Lazima uambiwe tena kwa lugha
inayoeleweka kosa ambalo unatuhumiwa nalo.
Unaweza kuambiwa kwa maandishi au kwa mdomo.
3. Una
haki ya kutaka kuitiwa mwanasheria , ndugu,
au rafiki ambaye unaamini atakusaidia
katika kutoa maelezo au kufanya mahojiano.
4. Ni kosa
kulazimishwa kukiri kosa au kuandika kile askari
anachotaka.
5. Baada
ya kutaja jina lako na anuani yako
una haki ya kutojibu swali jingine
ikiwa utaona inafaa kufanya hivyo.
6. Una
haki ya kukataa kujibu maswali yasiyo
na staha au yanayolenga kudhalilisha au
kuondoa utu wako au wa familia yako.
7.
Hairuhusiwi kupigwa, kudhalilishwa, kuteswa unapohojiwa
au unapokuwa kizuizini.
8. Una
haki ya kupatiwa au kuwezeshwa kupatiwa
matibabu ikiwa u mgonjwa au una jeraha wakati
wa mahojiano au kizuizini.
9. Ikiwa
aliyewekwa kizuizini ana umri chini ya
miaka 16 basi mara tu baada ya
kukamatwa kwake afisa polisi aliyemkamata au mwingine
ana wajibu wa kuhakikisha anawasiliana
na mzazi au mlezi na
kumweleza kukamatwa , kituo alipo, na kosa
alilokamatiwa.
10. Askari
anayekuhoji ana wajibu wa kuweka katika
rekodi/maandishi mahojiano yenu ili kusiwe
na kuongezwa au kupunguzwa kwa yale uliyosema.
11. Baada
ya mahojiano utatakiwa kupewa yale
yaliyorekodiwa/kuandikwa ili nawe uyapitie
kuona kama ulichosema kimekosewa au kiko
sahihi.
12. Ikiwa
kilichorekodiwa sicho ulichosema una haki
ya kumtaka aliyekuwa anarekodi/anaandika
kubadilisha eneo lilikosewa na kuandika upya
kile unachoeleza.
13. Kama
hujui kusoma basi unaweza kumtaka ndugu,
rafiki, au mwanasheria wako akusomee au
askari polisi akusomee ili uthibitishe usahihi wa
kilichoandikwa.
14. Iwapo
umekiri kosa na umesoma maelezo yapo
sahihi basi mwishoni utatakiwa usaini
uthibitisho maalum wa kukiri kosa.
15. Una
haki ya kuomba kuandika maelezo badala
ya kujibu kwa mdomo.
16. Ikiwa
utaomba kuandika basi ni wajibu wa polisi
kukuwezesha kwa vifaa vinavyohitajika ili uandike.
17.
Inaruhusiwa kuhojiwa masaa manne tu, isipokuwa
ikiwa ya kuhojiwa bado yapo muda huo
unaweza kuongezwa hadi masaa nane .
18. Masaa
manne ya mahojiano yanapoisha ni lazima
ziwepo sababu za msingi za kuongeza
masaa mengine. Si hiari ya polisi
kuamua bila sababu kuongeza muda wa
mahojiano.
19. Vitisho
na kumlaghai mtuhumiwa wakati wa kuhoji
haviruhusiwi. Mtuhumiwa atoe maelezo kwa hiari
huru(free consent).
20. Kabla
hujahojiwa una haki ya kuelezwa haki
zako ikiwemo ile ya kukaa kimya, ile
ya kuwa maelezo unayotoa yanaweza kutumika
mahakamani kama ushahidi ili uwe makini, na
nyingine zilizoelezwa humu
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni