Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo. |
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikagua baadhii ya maeneo ambapo michezo hiyo itafanyika. |
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa amegawa vifaa
mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo
huku akitaka michezo yote kuendelezwa.
Mgimwa ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali
vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika ziara yake inayoendelea
ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda
kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mgimwa
amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ili kutimiza ahadi yake kwa ombi la Vijana .
“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata. Lakini pia mimi
mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa na leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.”
Alieleza Mgimwa.
Mgimwa ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la
kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya kazi
zake kama Mbunge.
Ameongeza kuwa licha ya michezo kujenga utimamu wa mwili lakini pia
ni ajira huku akitoa mfano kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga
Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi na mipira
ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo
ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
Aidha,
amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani
yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku
kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao ambapo alisisitiza kuwa endapo michezo itaendelezwa
zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni