Gwiji wa muziki wa
taarabu Afrika mashariki MFALME MZEE YUSUF ameamua kuachana na mziki na
kumrudia Allah.
Mzee Yusuf ametangaza
Nia yake hiyo jana ijumaa tarehe 12-08-2016 Muda mfupi baada ya kumaliza
kuswali swala ya ijumaa katika msikiti wa Ilala bungoni (Masjid Taqwa).
Akizungumza huku akibubujikwa
na machozi mengi Mzee Yusuf amemuomba Allah amsamehe madhambi yake yote pamoja
na kuwaomba waumini wote wamuombee msamaha kwa Allah.
Pia amewaomba
wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao
walizonazo katika kutangaza na kusifia Shamaail za bwana mtume muhammad
(s.a.w).
Hata hivyo avitaka
vyombo vya habari vyote nchini na duniani sanjari na watu wote waliokuwa na Cd
zake majumbani mwao kuacha kupiga nyimbo zake ambapo amewatahadharisha kuwa
endapo watakaidi kufanya hivyo madhambi
yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah hivyo yeye hana
dhimma hiyo Tena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni