Na.Catherine Sungura,WAMJW-Kagera
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekataza
kulipisha pesa za vipimo kwa wagonjwa wote wenye kadi za bima ya afya
Waziri huyo ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi walioenda kupata matibabu kwenye kituo cha afya cha rwamishenye
"Ni
marufuku kuwalipisha wagonjwa wale wote wenye bima ya mfuko wa afya ya
jamii ama tele kwa tele au kadi za bima ya afya labla kama dawa hakuna
ndio wanaweza kununua"alisema
Aidha, amewataka
wananchi kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe hasa wale ambao hawajakata
tele kwa tele hasa vijijini ili waweze kupata huduma za afya bila kulipa
kila waendapo kupata huduma
"Mnajua hakuna
anayejua leo ama kesho ataugua,na magonjwa hayapigi hodi na wakati
mwingine yanakukuta hauna akiba ya fedha,ila ukiwa na bima wakati wowote
unapata matibabu"
Hatahivyo amewakumbusha watoa huduma za
afya kuweza kutoa huduma kwa kufuata kanuni na weledi wao ili kuweza
kuondoa malalamiko mengi toka kwa wananchi.
"Mgonjwa
anapofika kituo cha afya anakuwa aidha amechanganyikiwa au ana mawazo
mengi hivyo anahitaji kauli nzuri,faraja na huduma zinazostahili,hivyo
wakuu mganga mkuu wa kituo unatakiwa kukemea na kukumbusha maadili na
viapo vya maadili vya watoa huduma"
Aliwasisitizia
kuwa bima ya afya ya jamii inawahudumia wanachama sita kwenye familia
hivyo itawasaidia hasa pale mtoto anapotimiza umri wa miaka mitano hivyo
atahitaji kulipia huduma zote za afya.
Kwa
upande wa uzazi wa mpango Waziri Ummy aliwataka akinamama hao wazae kwa
kufuata uzazi wa mpango kwani maisha ya siku hizi ni magumu
"Hatusemi
kwamba mzae watoto wachache lakini mzae kwa mpangilio,'Mhe.Rais
amewezesha elimu bure" ila mtoto anahitaji malezi,maziwa pamoja na
malazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni