Waandishi wa habari
wanawake kutoka kutoka katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania wametembelea
hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo katika Mkoa wa Pwani,
Waandishi hao wapo katika ziara ya siku kumi ambapo watapata nafasi ya kutembelea baadhi ya hifadhi zilizopo nchini kama Saadani, Mikumi, Udzungwa na Ruaha.
Mhifadhi utalii Bi.Apaikunda Mungure kiwa ameongozana na wanahabari mara baada ya kuwasili katika hifadhi hiyo hivi karibuni. |
Akizungumza na wanahabari wanawake waliopo kwenye ziara hiyo,
mhifadhi utalii katika mbuga ya Saadani Bi. Apaikunda Mungule, amesema Saadan ni hifadhi pekee nchini ambayo inasehemu ya bahari ya Hindi jambo ambalo huwafanya
watalii wengi kufurahia na kuridhika na
huduma waipatayo pindi wanapotembelea hifadhi hiyo sanjari na utalii mwingine
kama utalii wa kupanda boti nk.
Akizungumzia kuhusu utaratibu unaotumika kukamilisha malipo
kwa watalii wa kigeni na watalii wa ndani wanaokwenda, Apaikunda amesema kwa sasa watalii wanatakiwa kwenda na kadi
ambazo hutolewa na CRDB, NMB na EXIM BANK.
Hata hivyo akafafanua kuwa dhumuni la kuweka utaratibu huo
wa kadi ni kumuepushia usumbufu mtalii
anaefika katika hifadhi hiyo pamoja na kukata kodi.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Saadan, bw. Lomi
Ole Meikasi, amesema hifadhi ya Saadani
ni moja kati ya hifadhi kumi na sita (16) zilizopo nchini Tanzania yenye sifa ya kipekee katika afrika mashariki
kwa kuwa inasehemu ya bahari ya hindi licha ya kuwa na mazingira ya kawaida
kama hifadhi nyingine zilizopo nchini.
Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Saadan na mhifadhi wa Ikologia, bw. Lomi Ole Meikasi akizungumza na wana habari ofisini kwake. |
Amesema hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1100 ni
hifadhi yenye umri mdogo ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2005 kwa tangazo rasmi la serikali namba 281
tarehe 16/9/2005, baada ya kulipandisha
hadhi lililokuwa pori la akiba la Saadani, na kwamba hifadhi hiyo ipo katika mikoa miwili
ya Tanga na Pwani huku ikiwa inazungukwa na wilaya nne ambapo
kwa upande wa Tanga hifadhi hiyo ipo katika wilaya za Handeni na Pangani na Pwani hifadhi hiyo ipo katika wilaya za
Chalinze na Bagamoyo na hiafadhi hiyo ina jumla ya vijiji 16 kwa Tanga na Pwani.
Akizungumzia idadi ya watalii, Kaimu huyo amesema kumekuwa
na ongezeko la asilimia themanini na nne (84%) tangu kuanzishwa kwake mwaka
2005 – 2015 ambapo idadi hiyo imeendelea
kukua kutoka watalii 3758 hadi
kufikia watalii 24145.
Kuhusu mapato amesema kuwa mwaka 2005 hifadhi hiyo
ilikusanya kiasi cha milioni arobaini na tisa na laki tatu tu (49,300,000/=) na
hdi kufikia mwaka 2015 hifadhi hiyo imekusanya zaidi ya bilioni moja na
ishirini.
Akizungumzia namna ambavyo hifadhi hiyo inashirikiana na
jamii katika kudumisha amani na ulinzi baina ya hifadhi na vijiji jirani vinavyo izunguka hifadhi
hiyo kwa lengo la kudhibiti vitendo vya
ujangiri pamoja na kutatua changamoto ya migogoro baina ya wanavijiji na
hifadhi hiyo bw. Mekasi amesema kuwa jumla ya sh. 722,830,000/= zimetumika
katika miradi mbali mbali ya kijamii kama ujenzi wa nyumba vya madarasa,
kuchangia madawadi katika shule za vijiji
katika mikao ya Tanga na Pwani nk.
Hifadhi ya Saadani ina jumla ya vijiji 16 ambapo
kwa upande wa Mkoa wa Tanga hifadhi hiyo
inapakana na wilaya za handeni na
Pangani ambapo Handeni ina vijiji 4 na
Pangani ina vijiji 7 na kwa upande wa Mkoa wa Pwani hifadhi hiyo inapakana na
wilaya za Chalinze na Bagamomo , mbapo Chalinze ina vijiji 2 na Bagamoyo ina
vijiji 3.
Picha: baadhi za vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo ya Saadani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni