Kushoto ni Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha, akizungumza na wanahabari hivi karibuni. |
Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw. Simon N. Naivasha, akiwaelezea jambo waandishi wa habari (hawapo pichani) |
Muhifadhi Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa Udzungwa bw.
Simon N. Naivasha mesema kuwa Hifadhi ya Taifa Udzungwa imechangia jumla ya madawati 1062 yenye
thamani ya sh. 128 milioni katika shule
za msingi 18 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu Wilayani
Kilombelo Mkoani Morogoro.
Akizungumza na wanahabari wanawake kutoka katika mikoa
mbalimbali nchini Tanzania ambao walitembelea hifadhi hiyo ya Udzungwa, Simon
amesema hifadhi hiyo imechangia kiasi hicho cha madawati kupitia mradi wa Ujirani Mwema na
kwamba madawati hayo yametolewa kwa
awamu tatu.
Akafafanua zaidi kuwa awamu ya kwanza Tanapa ilichangia
madawati 414 yenye thamani y ash. 56 milioni madawati hayo yalipelekwa katika
shule za msingi 17 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kidatu, awamu ya pili
madawati 278 yenye thamani ya sh.26 milioni ambayo tayari yamesha kabidhiwa
katika shule za msingi 18 zilizopo katika tarafa za Mang’ula na Kitatu , na
awamu ya tatu ni madawati 370 yenye thamani y ash. 46 milioni ambayo
yatakabidhiwa hivi karibuni baada ya kukamilisha taratibu za kukabidhi kwa
shule 18 ambazo zipo katika tarafa za
Mang’ula na Kidatu Wilayani Kilombelo mkoani Morogoro.
Navasha akaongeza kuwa
TANAPA ilianza mchakato wa kuchangia madawati katika vijijini
vinavyopakana na hifadhi ya Udzungwa tangu mwaka 2013 ambapo alibainisha kuwa miongoni mwa
vigezo ambavyo vinatumika katika kuchagua ni kijiji ama shule gani zipewe madawati au miradi mingine yenye lengo ya kuwasaidia
wananchi waishio katika vijiji vinavyo pakana na hifadhi hiyo ni
pamoja na kuangalia vijiji ambayo vimekuwa vikitii sheria za uhifadhi bila
shuluti kama kushiriki kutoa taarifa za ujangili, kuto kata miti, kuto choma
moto, kutofanya shuhuli za uwindaji
ndani ya hifadhi nk.
Hata hivyo Naivasha amesema kuwa ipo miradi mingi ya ujirani
mwema, miongoni mwa miradi hiyo ni pamoaja na ujenzi
wa vyumba vya madarasa,ufugaji wa kuku hususani kwa wakina mama, ufugaji nyuki,
ufugaji ngombe na mbuzi, ambapo miradi ya ufugaji imeanzishwa katika maeneo
ambayo wakazi wake hususani wanaume walikuwa wakijihusisha zaidi na shughuli za
uwindaji ndani ya hifadhi.
Naivasha amefafanua kuwa dhumuni la kuanzisha miradi ya
ujirani mwema ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa ni kuondoa migogoro baina ya
wakazi waishio maeneo ya karibu na hifadhi na Tanapa, kuimarisha kudhibiti wa
vitendo vya ujangili, kwani kupitia
miradi hiyo Tanapa inapata nafasi ya kutoa elimu kwa wananchi kila inapobidi
kufanya hivyo.
Akizungumzia changamoto ambayo Tanapa inakumbana nayo katika kutekeleza miradi hiyo ya ujirani
mwema, ‘’changamoto kubwa tunayo kabiliana nayo ni ugumu wa wananchi kuchangia
ile asilimia ndogo wanayopaswa kuchangia, mnajua kwa kawaida Tanapa tunachangia
70% na wananchi nao wanatakiwa kuchangia 30% lakini wanakuwa wagumu kutoa”
alisema Naivasha.
Kuhusu sababu zinazopelekea wananchi hao kuwa wagumu
kuchangia hata kwa kiasi kidogo wanachopaswa kuchangia Naivasha amesema ni
matumaini makubwa ya wananchi. “unajua wananchi wengi wanaamini kuwa Tanapa ina
hela nyingi sanaa pia hela hizo zinatolewa na serikali, hivyo kuna tunapata
changamoto kubwa sana tunapoenda kukabidhi miradi hiyo ukiwaambia wanatakiwa
kuchangia wanaona kama wewe ulieenda kukabidhi
mbaya hivyo wananchi wanamatumaini makubwa kupita kiasi hiyo ndiyo
changamoto” alisema Naivasha.
Alimaliza kwa kutoa wito kwa wananchi waishio maeneo jirani
na hifadhi kutambua kuwa jukumu la kuzilinda hifadhi nila kila mwananchi pia
akawataka washiriki vema katika kuisaidia Tanapa kupambana na vitendo vya
kijangili ambavyo vinashamiri kwa kasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni