Mbunge Joseph Mbilinyi (SUGU), akizungumza na wanahabari mkoani Mbeya kuhusu ajali hiyo. |
Gari la mbunge Joseph Mbilinyi (SUGU) baada ya kupata ajali.
|
Gari la Mbunge wa Mbeya mjini
Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, limepata ajali na kusababisha kifo
cha mtoto wa miaka 13 mwanafunzi wa shule ya sekondari Lupato.
Ajali hiyo imetokea jana asubuhi
majira ya saa 2:00 asubuhi ambapo gari lenye namba za usajili T161 CPP mali ya
mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ambalo lilikuwa likiendeshwa na Gabriel
Andrea (43) mkazi wa Mwakibete, lilifeli break na kusababisha kifo cha mtoto
Rahel/Rachael Lutumo ambae alikuwa
akivuka bara bara Iyunga katika eneo la kuvukia watembea kwa miguu (zebra).
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
kaimu kamishna Dhahir Kidavashari, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba mtoto Rahel Lutumo alifariki njiani wakati akikimbizwa Hospital ya Rufaa
Mbeya kwa ajili ya kupatiwa matibabu na mwili wake kuhifadhiwa katika hospital
ya Rufaa Mbeya na kwamba dereva wa mbunge Sugu anashikiliwa na jeshi la polisi kwa
mahojiano zaidi.
Kwa upande wake mbunge Joseph
Mbilinyi maarufu kwa jina la SUGU ambae
hakuwa tayari kuzungumza na wanahabari ili kuizungumzia ajali hiyo amesema
amesikitishwa na ajali hiyo ambayo imepoteza maisha na mwananchi ambae hana
hatia.
Akizungumzia madai ya gari lake
kukimbia eneo la tukio baada ya kusababisha ajali hiyo jambo ambalo lilipelekea
gari lake kufukuziwa na madereva bodaboda na hatimae kurudi eneo la tukio ,
Mbunge huyo amekanusha madai hayo na
kusema kuwa sababu iliyopelekea kushindwa kusimama mara baada ya tukio hilo ni
kutokana na gari lake kufeli break hivyo haikuwa rahisi kusimama na si
vinginevyo.
Wakati huohuo askari wa nne wa
usalama barabarani wamenusulika kifo baada ya gari walilokuwa wakilitumia kupinduka katika eneo la Isanga (bara bara ya kuelekea
Chunya)
Gari hilo lilikuwa likijaribu
kuwahi eneo la tukio Iyunga eneo ambalo
mtoto Rahel Lutumo aliyegongwa na gari la mbunge Sugu na kufariki dunia wakati
akipelekwa hospital kupatiwa matibabu.
Kamanda wa polisi Dhahir Kidavashari akifafanua kuhusu ajali mbili tofauti zilizotokea mkoani Mbeya. |
Gari la Mbunge Sugu. |
Gari la polisi linalotumiwa na askari wa usalama barabarani katika eneo la tukio Isanga (barabara ya Chunya) Mbeya. |
Gari la polisi linalotumiwa na askari wa usalama barabarani likikokotwa. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni