Shirikisho
la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya leo limefanya
kikao cha kuadhimia kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ndg. Alex
Julius Kinyamagoha kwa madai ya kukosa imani nae baada ya mwenyekiti huyo kuandika waraka na
kuusambaza katika mitandao ya kijamii Facebook na WhatsApp .
Katika
waraka huo Ndugu Alex Kinyamagoha anadaiwa kuandika waraka unaopinga mabadiliko
yaliyojadiliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa sanjari na kuwakashfu mwenyekiti
CCM Taifa aliemaliza muda wake madarakani Ndg, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na
Mwenyekiti CCM Taifa aliyopo madarakani sasa Mh. Rais John Pombe Magufuli na
kuusambaza katika mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wake wa Facebook na Whatsapp
mnano tarehe 15/12/2016.
Akizungumza
katika mkutano huo ndg. Frank Boaz ambae ni mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa
amesema kuwa kitendo alichofanya Alex Kinyamagoha kinaashiria dhahiri kuwa alitumwa
hivyo chama cha CCM hakiwezi kamwe kuwavumilia mamluki kwa namna yoyote kwani
shirikisho litajengwa na wanachama wenye nia njema hivyo shirikisho halitasita
kuwaondoa mamluki na tayari shirikisho hilo limeanza na Alex Kinyamagoha.
Naye Katibu
wa Siasa na Uenezi Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya ndg. Oddo Aidan
Ndunguru, amesema kuwa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya limekerwa na
waraka huo na ambapo aliwataka watanzania waupuuze waraka huo na watambue kuwa waraka
huo ni mawazo binafsi ya ndg Alex Kinyamagoha na si Shirikisho kwani Shirikisho
halijawahi kufanya kikao cha kujadili mabadiliko yaliyo pendekezwa na
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Hata hivyo
akatumia nafasi hiyo kuwaomba radhi viongozi wote wa CCM na ngazi zote,
wanashirikisho na wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi kote nchini ambapo
alisema kuwa Shirikisho hilo linaunga mkono mabadiliko yaliyojadiliwa na Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa pamoja na uteuzi wa viongozi uliofanywa.
“hakuna haja
ya kuendelea kuimba CCM iyena iyena wakati mapenzi yako yapo nje ya chama hivyo
ni bora ukatoka ukaenda huko ambapo una mapenzi napo, lazima tutambue kuwa kama
watangulizi wetu wangefanya makosa CCM isingekuwepo leo hivyo ccm haita
wavumilia mamluki kwa namna yoyote ni lazima watoke”.
Nduguru
akamaliza kwa kusema nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya
juu Mkoa wa Mbeya itakaimiwa na Ndg. Michael Malegesi hadi hapo uchaguzi wa
kuziba nafasi hiyo utakapo fanyika, na kwamba shughuli zote za Shirikisho zitaendelea
kama kawaida.
Ikumbukwe kuwa Ndg. Alex Kinyamagoha aliandika
waraka huo na kuusambaza katika mitandao ya kijamii Facebook kupitia ukurasa
wake na WhasApp mnamo tarehe 15/12/2016, na manamo tarehe 16/12/2016 majira ya
11:51 usiku akaomba radhi kwa waraka huo katika mtandao wa kijamii wa facebook
kupitia ukurasa wake uliosomeka kama ifuatavyo...
Aliekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu la Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya. |
Katibu wa Siasa na Uenezi Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya ndg. Oddo Aidan Ndunguru. |
Frank Boaz Mjumbe akizungumza katika mkutano huo. |
Michael Malegesi Kaimu Mwenyekiti Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, akizungumza katika mkutano huo |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni