Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kizota
Manispaa ya Dodoma, Yassin Abdallah (13) amejinyonga kwa kutumia shuka la
bafuni baada ya kupata matokeo mabaya ya mitihani yake ya mwisho wa mwaka.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Ernest Kimola,
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea siku tatu zilizopita majira ya mchana katika
mtaa wa Kizota Relini, Manispaa ya Dodoma.
Kwa mujibu wa Kamanda Kimola amesema baba mzazi wa marehemu
Hassan Juma mwenye umri wa miaka 53 aligundua kuwa mwanae amejinyonga kwa
kutumia shuka,
Nae diwani wa Kata ya Kizota, Yaredi Jamal, amesema siku ya
tukuo alikuwa kwenye kikao akapokea simu kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa akimtaarifu
kuwa mwanafunzi huyo amejinyonga, na kuongeza kuwa kwa mujibu wa wazazi wa mtoto
huyo, alikuwa ana miezi miwili tangu ahamie katika shule hiyo akitokea mkoani Kigoma.
Inadaiwa mtoto huyo katika matokeo yake ya mwisho alishika
nafasi ya 128 kati ya wanafunzi 132, hali ambayo ilimstua na kuamua kujinyonga
“hapo shuleni kaanza masoangemo mwezi wa 11 kwa mujibu wa
walimu, ambapo kila akifundishwa na walimu alijiona haelewi kutokana na
kuwakuta wenzake wakiwa wamemtangulia katika masomo wanayofundishwa,” alisema
diwani Jamal.
Kufuatia hali hiyo, Diwani Jamal alitoa rai kwa wazazi kuwa
karibu na watoto wao na kuepuka kutoa vitisho ambavyo vitawasabisha wachukue
maamuzi magumu.
“Nimeongea na wazazi
wanasema hawajawahi kuzungumza lolote na walitambua mtoto wao anatoka kijijini
anakuja kukutana na watoto wa mjini ambao uelewa wao ni tofauti, Walitarajia
hadi mwakani mtoto wao angekuwa ameanza kuelewa masomo aende sawa na wenzake,”
alisema Diwani Jamal.
Diwani Jamal alisema tukio hilo limemsikitisha na halijawahi
kutokea mtoto mdogo kufikia uamuzi wa aina hiyo, hivyo ni vyema wazazi wakawa
karibu na watoto wao kitaaluma.
chanzo: Nipashe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni