Nyumba iliyokuwa ikitumika kama kilabu ikiwa imebomoka baada ya kugongwa na lori |
lori la mizingo lenye namba za usajili T801 ACD,lililo sababisha ajali na vifo vya watu 5 |
Ajali iliyo sababisha vifo vya watu 5, imetokea usiku wa leo mkoani Iringa baada ya lori la
mizingo lenye namba za usajili T801 ACD lililokuwa likielekea mkoani Mbeya
kuacha njia na kugonga kilabu cha pombe za kienyeji.
Tukio hilo limetokea majira ya saa nne kasoro usiku wa leo
katika eneo la njia panda Makumbusho ya Isimila kata ya Mseke barabara kuu ya
Iringa-Mbeya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio wanasema watu hao watano
wakiwemo ndugu watatu waliku ndani ya kilabu hicho wakiendelea kunywa pombe za
kienyeji wakati ajali ikitokea,
mashuhuda hao wamesema lori hilo liliacha njia na ghafla lilienda kugonga
nyumba ambayo ilikuwa ikitumika kama kilabu cha pombe za kienyeji na kwamba
wakati ajali hiyo inatokea baadhi ya wateja walikuwa nje ya kilabu hicho hivyo
waliliona lori hilo ambapo walianza kukimbia huku wakipiga kelele ili
kuwasaidia waliopo ndani lakini hawakufanikiwa kukimbia.
Kwa mujibu wa Jeshi la polisi waliopoteza maisha ni leonard
Mkendela (35), Neema Mkendela, Kamsia Mkendela wote wa familia moja na wengine
ni Ester Mwalomo na Oscar Zosama (25) wote wakazi wa Isimila.
Majeruhi wa ajli hiyo Kasimu Ahmed Mambo (44), mkazi wa
Kijiweni pia ni dereva wa lori hilo, Mussa Abdalah (34) mkazi wa kijiweni pia
ni utingo wa lori lililopata ajali na Juma Abdalah omary Ally (40) ambae
anadaiwa kuwa ndie alikuwa akiendesha lori hilo lililo sababisha ajali.
Wengine walio nusurika katika ajali hiyo ni muuzaji wa
kilabu hicho ambaye wakati ajali inatokea alikuwa ameenda msalani nyumba ya
jirani iliyo karibu na kilabu hicho.
Dereva wa lori bw. Kasimu Ahmed akipelekwa wodini katika Hospital ya Rufaa mkoa wa Iringa |
Majeruhi Musa Abdalah (34)ambe ni tingo wa lori lililo sababisha ajali |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni