Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Claud Gwandu |
Katika hali ya sintofahamu mapema leo jijini Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia kusanyiko la watu walioongozwa na mstahiki Meya wa jijji la Arusha Kalisti Lazaro Bukhay, kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba katika ajali uliyopoteza uhai wa dereva, walimu na Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.
Tukio hilo kwenda kutoa rambirambi pia lilihudhuriwa na Madiwani, viongozi mbalimbali wa dini pamoja na waandishi wa habari lilikuwa
likiendelea kufanyika katika eneo la shule hiyo ambapo ghafla polisi walifika na kuwaweka chini ya ulinzi.
Inaelezwa
kuwa baada ya polisi hao kuwaweka chini ya ulinzi waliondoka nao wote wakiwemo
Waandishi wa habari wapatao kumi, lakini katika hali ya kushangaza baada ya
kufika kituo cha polisi cha kati polisi hao waliwaachia huru waandishi kwa
madai kuwa hawana shughuli nao bali waliwapa lift tu kutoka kwenye eneo la
tukio hadi kituoni hapo.
Hata
hivyo katika mkutano uliofanyika dakika chache baada ya waandishi hao kuachiwa
huru, Polisi walidai alie amuru polisi kuwashikilia wote waliokuwa
wamekusanyika kwa lengo la kutoa
rambirambi hakujua kama kulikuwa na waandishi na kwamba hawakuwa na kosa lolote na ndio maana
waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.
Kufuatia
tukio hilo,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imelaani tukio
hilo.
Katika hatua nyingine meya wa jiji la Arusha, madiwani, walimu, mmiliki wa
shule ya lucky Vincent, viongozi wa dini waachiwa huru kwa dhamana kwa sharti la
kufika kituoni hapo kila watakapoitajika kufanya hivyo.
Shule ya lucky Vincent lipata pigo mnamo may 6.2017 majira ya saa 4 asubuhi
kufuatia ajali iliyotokea katika eneo la
Rhotia wilaya ya Karatu na kusababisha vifo zaidi ya 30 vikiwahusisha wanafunzi, walimu na dereva, ajali
hiyo ilitokea wakati wakielekea kushiriki
mtihani wa kirafiki wa moko na wenzao wa shule ya msingi Tumanini Junior
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni