Wananchi waliokuwa wakiishi katika Hifadhi hiyo wakiendela kuokoa mali zao wakati wa zoezi la kuwaondoa. |
Mmoja ya wananchi aliyejitambulisha kwa jina la mtoto wa Singinda yatima akilia kwa uchungu baada ya nyumba yake kuteketezwa kwa moto katika operation ya kuwaondoa wavamizi wa Hifadhi za Misitu. |
Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya Mh. Mkuu wa Wilaya Rehema Madusa akiendelea na zoezi la kuchoma nyumba katika operation ya kuwaondoa wavamizi wa Misitu. |
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Rehema Madusa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusiana na madai ya wananchi (wavamizi) kuchangishwa fedha ili wasiondolewe katika Hifadhi hiyo. |
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Chunya Grace William, akitolea ufafanuzi kuhusu zoezi hilo. |
Zaidi ya watu 900 wamepoteza makazi
yao baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wakishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS) katika Halmashauri ya
Wilaya ya Chunya kuendesha zoezi (operation) la kuwaondoa wavamizi waliokuwa
wamejenga makazi na kufanya shughuli za uzalishaji ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Asili uliyopo katika
Tarafa ya Kipembawe katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Baadhi ya wananchi hao jamii ya
wafugaji waliokumbwa na kadhia hiyo ya kubomolewa na kuchomewa nyumba zao kwa
moto wameelezea kushangazwa zoezi hilo na wengine wakiangua kilio na kuwalalamikia
baadhi ya viongozi kwa kuwahakikishia kuwa wapo salama na kuwataka kuendeleza
shughuli za uzalishaji sanjali na kuendelea kuwauzia maeneo na kuwatoza fedha kiasi cha shilingi elfu sabini (70,000) kwa
kila kaya madai kuwaa fedha hizo zilikuwa zikitumika kwa ajili ya kuwashawishi
viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ili wasitishe zoezi la kuwaondoa katika
maeneo hayo.
Zoezi la kuwaondoa wafugaji
limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh. Rehema Madusa ambae amekiri kuwepo
kwa taarifa za baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu waliokuwa wakiwachangisha
fedha wafugaji hao kwa njia za udanganyifu kupitia mgongo wa Serikali kuwa
hadaa kuwa zoezi la kuchangisha fedha hizo lilikuwa ni utekelezaji wa agizo la
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya na kwamba dhumuni la kuchangisha
fedha hizo ni kuwatuliza viongozi ili wasitishe mpango wa kuwaondoa wavamizi.
Mh. Madusa ameongeza kuwa baada
yakupata taarifa hizo ofisi yake ilichukua hatua za kwenda kuchunguza madai
hayo na kwamba kufuatia tuhuma hizo
Jeshi la Polisi Wilayani humo linawashikilia watu wawili kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
Akielezea kuhusu maandalizi ya awali yaliyofanyika hadi kufikia hatua ya maamuzi ya kwenda kuteketeza kwa kuchoma moto nyumba zaidi ya 900 za wananchi jamii ya wafugaji ili kuwaondoa
katika maeneo hayo Madusa amesema Serikali ili anza kwa kutoa elimu kwa
wananchi hao na kisha kutoa notisi (notice) ya miezi mitatu ya kuwataka kuondoka katika maeneo hayo lakini wafugaji hao hawakuzingatia na kutiii maagizo ya Serikali na ndipo zoezi hilo likaamriwa kufanyia.
Meneja wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Chunya Grace William amesema Tarafa ya
Kipembawe kuna Misitu zaidi ya saba inayohifadhiwa yenye ukubwa wa hekta zaidi
ya laki mbili lakini misitu hiyo
imevamiwa na makundi ya watu ambao wanaendesha shughuli za kiuchumi kama
Kilimo, Ufugaji, Uchimbaji na kusababisha uharibifu wa mazingira na kuongeza
kuwa zoezi hilo la kuwaondoa wavamizi wa misitu ni endelevu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni