Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. |
Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo. |
Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo. |
Jumla ya wadadisi 600 wamepatiwa mafunzo ya
siku 5 kwa ajili ya kufanya Utafiti wa
Kilimo wa mwaka
2016/17 nchi nzima kuanzia Oktoba hadi 3 Novemba, 2017 nchi nzima.
Takwimu hiyo imetolewa
na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa mjini Dodoma wakati wa kuhitimisha mafunzo
hayo na kuongeza kuwa madhumuni ya mafunzo kwa wadadisi hao ni kuwajengea uwezo
wa kuhoji na kujaza madodoso ya wamiliki wa mashamba (wakulima) na namna ya
kutambua mahali shamba lilipo kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho GPS.
Utafiti huu wa Kilimo
wa mwaka 2016/17 unafanyika chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi
ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar (OCGS) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo amesema lengo la utafiti huo ni
kutoa makadirio ya kiasi cha uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo, mazao
yatokanayo na mifugo na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya Tanzania.
Aidha, Mashingo ametoa wito kwa wakuu wote wa kaya watakaochaguliwa
kushiriki kwenye utafiti huu, kutoa
ushirikiano wa kutosha hususan taarifa sahihi kuhusu hali ya uzalishaji wa
mazao, huduma zinazotolewa na Maafisa Ugani na aina ya mbegu wanazotumia na
kubainisha changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni