picha hii sio halisi |
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Julius Kaondo amewatahadharisha wazazi na walez kuwa watamuona mbaya iwapo watashindwa kuwapeleka watoto wao shule kwa madai kuwa hawana uwezo.
Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni alipokuwa akisalimiana na wananchi katika ibada maalumu ya kuiombea Serikali ya Awamu ya Tano sambamba na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 kwa amani na utulivu .
Kaondo alisema kuwa idadi ya watoto waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari mwaka huu wilayani Nkasi ni 2,274 sawa na asilimia 67.38.
“Watoto hao wote waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka huu lazima waende kuripoti shuleni kwa hakuna sababu ya mzazi au mlezi kushindwa kumpeleka mtoto wake shule kwa maana tayari Serikali imeondoa ada na michango shuleni kwamaana hiyo elimu ni bure kuanzia shule ya awali hadi Kidato cha Nne “ alisisitiza
Ameongeza kuwa yeye binafsi hatakua na huruma kwa mzazi yeyote atakayezembea kumpeleka mtoto wake shule na kuwa watendaji wa vijiji na kata watapewa orodha ya watoto hao na watakua na wajibu wa kuhakikisha kuwa kila mtoto aliyefaulu kuendelea na masomo amekwenda shule ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kutekelezaagizo lake hilo .
Aidha amewataka wazazi wenye watoto wanaostahili kuanza darasa la kwanza mwaka huu wawe wameandikishwa kuanza darasa la kwanza mapema Januari na
Alisema kuwa wazazi katika halmashauri hiyo wamekuwa wakishindwa kuwapeleka watoto wao darasa la kwanza na wengine kidato cha kwanza kwamadai kuwa hawana uwezo wa kuwasomesha watoto hao wakidai gharama kuwa kubwa.
“ Natoa onyo kwa mzazi yeyote atakaye shindwa kumpeleka mtoto wake shule kwani serikali imesha mgharamia kila mwanafunzi kuanzia wa darasa la kwanza mpaka wa kidato cha nne sasa ole wake mzazi atakaye acha mtoto wake ashindwe kwenda shule….nawaambia tutaonana wabaya ifikapo Februari ”…. Alisema mkurugenzi huyo
.
Alisema tatizo jingine lililopo wilayani humo ni idadi kubwa ya wanafunzi kukatiza masomo yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro , mimba na ndoa za utotoni .
Akitoa mfano alisema wanafunzi wapoanza darasa la kwanza mwaka 2009 wilaya nzima walikuwa 9,600 lakini ni wanafunzi 3,452 tu waliomaliza darasa la saba mwaka 2015 .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni