Ijumaa, 15 Januari 2016

KUKU WA AJABU AWALIZA WANA VIKOBA AIBA PESA KISHIRIKINA WILAYANI RUNGWE JIJINI MBEYA,

Wana kikoba cha Mwijangasyege wakiwa eneo
la kilabu cha pombe 
wakijadilian
kuhusu sintofahamu hiyo ya  kuku wa ajabu
 kukwapua pesa kimazingara

Hao ni miongoni mwa wanakikundi wa Kikoba
na huyo aliepo katikati ni bi. Basimenye
 Silimani ambae ndie katibu wa kikundi!



WANAKIKUNDI wa  kikundi  cha  kuweka  na kukopa maalufu kama VICOBA kijulikanacho kwa jina la Mwijangasyege  kilichopo kata  ya Isange wilayani  Rungwe mkoani Mbeya  , wameingia  kwenye  hali ya sintofahamu  baada  ya   pesa   zao kukwapuliwa  na  kuku kwa  njia ya   kishirikina.

Wakiongea  na Blog hii kwa  masikitiko makubwa ,  walisema tukio hilo la kusikitisha   lilitokea  wakati  wa mahesabu  ya  fedha hizo,  ambapo  katika hali ya kushangaza na kutatanisha  alitokea  kuku mweupe  na kudonoa fedha  kiasi  cha  shilingi laki nne  na  thelathini  na kisha kutokomea  kusikojulikana.

mmoja wa wanakikundi aliejitambulisha kwa jina la Hamu  Kitaje alisema   wanashindwa  kuelewa juu  ya kilichokuwa nyuma   ya  kuku huyo ambaye alifika eneo la tukio kama mwewe na  kukwapua pesa na kisha kutokomea nazo.

‘’Ilikuwa   hali   ya  taharuki, majira  ya  saa kumi na moja  jioni wakati tukiwa   katika  mahesabu ya  fedha   ambazo  tulitaka kugawana lakini  wakati  tukiendelea na zoezi hilo kufumba na kufumbua alitokea  kuku  mweupe  huku akiwa anarukaruka mithili ya mwewe,  kuku huyo akafika eneo la tukio na kutua pembeni huku akituangalia na kukodolea macho bulungutu la pesa, ambapo baada  ya  kumaliza kazi ya kuhesabu  fedha  zote  tukaziweka kwenye ungo  nandipo ghafla kukatokea hali kama ukungu hali iliyotufanya tusijue kinachoendelea na sekunde chache baadaye tulipigwa butwaa baada ya kuona pesa hazipo ’’Alisema kitaje.

Akifafanua kuhusu tukio hilo, Katibu  wa  kikundi  hicho ,Basimenye silimani ,alisema  jumla  ya  pesa  ilikuwa ni shilingi za kitanzania milioni mbili  laki nne na tisini elfu,  ambapo kati ya pesa  hiyo,  shilingi  laki nne  na thelathini ndizo  zilizo  kwapuliwa  na  kuku huyo na kusababisha sintofahamu kubwa miongoni mwao .

Aidha katibu huyo alisema  mpaka  sasa  hawaelewi   cha  kufanya  na badala  yake  wanaendelea  kusuburi  kitakachojili  kwani wanamtegemea  mungu  kama  ndie muweza wa  yote,‘’kama  wanakikundi  hatujaenda  kokote  kwa  ajili  ya  kupata uvumbuzi na kujua  kulikoni  kuhusiana  na kuku huyo  na  hivyo tunamwachia  mungu mwenyewe’’ alisema   silimmani,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni