Jumatano, 13 Januari 2016

VIONGOZI WA BARAZA LA VIJANA (BAVICHA) NA WANACHAMA WAFUNGA OFISI ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO WILAYANI KYELA


BAVICHA wakijadiliana jambo baada ya kufunga ofisi



VIONGOZI na wanachama wa Baraza la vijana BAVICHA wilayani Kyela
Mbeya,wameitaka kamati tendaji ya wilaya ikiongozwa na mwenyekiti wa
chama hicho,Sadat Daud,kujiuzuru ikiwemo kuwaomba radhi wanachama kwa
kuwatolea maneno ya fedhea ikiwemo kuwaita wahuni.

Kauli hiyo imetolewa siku  chache  kwenye kikao cha ndani
kilichoitishwa na Baraza hilo kilichokuwa na ajenda ya kuwajadiri
viongozi hao ambao wanadaiwa kukaidi agizo la wanachama ambao waliwapa
siku kumi na nne kuitisha mkutano mkuu kujadili muenendo wa uchaguzi
mkuu uliofanyka  wa mwaka jana 2015.

Viongozi wa wilaya wa chama hicho,wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya
ikiwemo kukihujumu chama pamoja na kushindwa kumsaidia aliyekuwa
mgombea ubunge wa jimbo hilo,Abraham Mwanyamaki aliyefungua kesi ya
kupinga matokeo ya ubunge wa Dr,Harrion Mwakyembe mahakama kuu kanda
ya Mbeya.

Grees Ngairo Mwenyekiti ambae ni Bawacha kata ya Bondeni,alisema mwenyekiti wa Chama wilaya Sadat Daudi na timu yake wajiuzuru kwani wamekihujumu
chama pamoja na kumtalekeza Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo
hilo,wakiendekeza maslahi binafsi huku wakileta mipasuko ndani ya
chama.

Furaha Amos mwenyekiti katibu na uenezi kata ya Itunge alisema
mwenyekiti wa chama wilaya na timu yake hawajaanza leo kukihujumu
chama,wamekuwakuwa wakiendekeza masrahi binafsi.

Esaya Mwakalobo,mwenyekiti Bavicha kata ya Mbugani,alisema mwenyekiti
wa wilaya hana busara,ambapo walimtaka aitishe mkutano mkuu ndani ya
siku 14 ili wajadili mustakabari wa chama.lakini amepuuza agizo hilo
na kuwaita wahuni na kuwa anatakiwa apokonywe kadi.

Alisema Bavicha walikaa kikao tarehe 4 ambapo licha ya kujadili mambo
kadhaa pia waliafikiana kuifunga ofisi wakishinikiza kamati tendaji
ijiuzuru kwa tuhuma mbalimbali ambapo kamati tendaji ilivunja mirango
hiyo na kuwa kwa sasa wanaifunga tena na kuweka ulinzi wakitaka
uongozi wa mkoa kuingilia kati.

Danis Maria mwenyekiti wa Baraza hilo,alisema kutokana na uongozi wa
wilaya kutowatendea haki wanachama,kamati tendaji yote inatakiwa
kujiuzuru akiwemo yeye ili kupishwa wengine watakao Kilejesha Chadema
kwenye uhai.

Alisema kesi iliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya Mbeya ilikuwa
nyepesi,uhakika wa kushinda ulikuwepo,kilichopelekea kesi hiyo ifutwe
ni kwamba chama kilimtelekeza aliyekuwa mgombea wa chama hicho,Abraham
Mwanyamaki kwa kutompa ushirikiano.

Bavicha wamefanikiwa kuifunga ofisi hiyo,na kuweka ulinzi,wakitaka
uongozi wa mkoa wa Mbeya ufike na kuweka viongozi wa muda,huku
wakimtuhumu mwenyekiti kukihujumu chama kwa madai alikuwa akitumika na
chama cha mapinduzi,huku katibu wakidai hakuwa na sifa za kuongoza na
kupelekea kupoteza ushindi.

Mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo,Sadat Daud,alisema vikao
vilivyokaliwa na baraza hilo, ni batiri na kuwa alishindwa kuitisha
mkutano mkuu kwa madai Kyela ilikumbwa na ugonjwa wa mlipuko wa
kipindupindu na kudai ilikuwa ngumu kukaidi amri ya serikali iliyopiga
marufuku mikusanyiko.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni