Jumatatu, 11 Januari 2016

MDUDU AINA YA PANZI AWA TISHIO KWA WAKULIMA WA RUNGWE MKOANI MBEYA


Picha ya zao la mahindi yaliyo haribiwa na ugonjwa huo ambao bado haujajulikana



WAKULIMA  wa mazao ya  chakula  katika  halmashauri  ya  Busokelo
wilayani Rungwe  mkoani mbeya  wameingia  kwenye  wakati mgumu  na
wasiwasi  baada  ya  mazao  yao  kuvamiwa  na  ugonjwa   usiokuwa  na
dawa   wala  kinga .

Wakiongea   na blog hii kwa  nyakati  tofauti , walisema  mazao yao   hasa
mahindi  yamevamiwa  na  ugonjwa  ambao  unapelekea  kunyauka  kwa
mimea  , ambapo kutokana na  hali  hiyo walisema wanawasiwasi mkubwa
kuhusu namna watakavyoishi  kwani   ndio  zao  ambalo   linategemewa
kwa  chakula ,ambapo  pia  walisema  linawapatia   kipato kwa ajili ya
kukidhi  mahitaji ya  familia.

Elia Mwakyoma mmoja wa wa wakulima maalufu wa zao hilo akizungumza na blog hii kwa
masikitiko makubwa ,alisema kwa mara  ya kwanza  ameshangazwa  na
matokeo ya  ugonjwa  huo  mara  baada ya  kuona  mahindi  shambani
kwake  yakinyauka  kwa kasi na kuongeza  kuwa   anawasiwasi  huenda
mwaka  huu  wasiweze  kuambaulia  chochote toka  mashambani ,hali
ambayo  inatishia usalama wa chakula na kusisitiza kuwa maisha ya
familia zao yataathilika  vibaya sana kutokana na hali hiyo.

Aidha kutokana na hali hiyo wakulima katika halmashauli hiyo wameiomba
serikali kutafuta uvumbuzi wa tatizo hilo na kuonya   kuwa vinginevyo
watakabiliwa na  janga  kubwa la njaa  kwani mahindi ndio  zao kubwa
linalotegemewa haswa kwa chakula.

Stivini mapunda ambae  ni afisa  kilimo  wilayani  humo , alikili
kuwepo  kwa   ugonjwa  huo  na kusema  unaenezwa  na  panzi . Aidha
aliwataka  wakulima   kupanda  mazao  mbadala ilikukabiliana na
tatizo  la  njaa  na kuwashauri  wakulima   kutumia   mbegu  mbadala
za  mahindi  ambazo  zinaweza   kuhimili  ugonjwa  huo.

‘’ugonjwa  huu  unasambazwa  na panzi  na  wala   hauna  dawa  wala
hatuwezi  kuzuia  kwasasa, hivyo ni  vyema wananchi    wakaanza
kujiandaa kupanda mazao  mbadala ili kukabiliana na  tatizo  la  njaa,
pia ili kupunguza kasi  ya kuenea   kwa  ugonjwa  huo shambani  ni
vyema wakulima  wakang’oa  na kuchoma  mimea  ilioathilika na ugonjwa
huo. Alisema  mapunda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni