Jengo la bunge la Malawi |
Jeshi
la polisi nchini Malawi lina washikiria baadhi ya viongozi wa chama cha upinzani
cha Malawi Congress Party MCP kwa ya kujadiliana/kupanga njama za kumuondoa
madarakani rais wa inchi hiyo Mutharika,
Msemaji
wa jeshi la polisi nchini Malawi Nicholas Gondwe amedhibitisha kukamatwa kwa Msemaji
wa chama cha Malawi Congress Party MCP, Bi. Jessie Kabwira ambae pia ni mbuge,
Mwasheria
wa chama hicho Bw. Peter Chakhwantha ambae pia ni mbunge pamoja na wengine wanadaiwa
kupanga njama za kumpinduwa rais Mutharika,
Bw.
Peter na wenzie inasemekana walikua wajadili Njama hizo kupitia Mtandawo wa
kijamii wa WhatsApp,
Kabwira
alikamatwa na jeshi hilo mita 500 nje ya ubalozi wa Ujerumani ambao hauko mbali
jengo la bunge la Malawi, wengine ambao ni Alekeni Menyani wabunge hao
walikamatwa wakati wakiwa katika harakati za kutafuta hifadhi katika ubalozi
huo wa Ujerumani.
Hadi
habari hii inawekwa mtandaoni katika blog hii kwa mujibu wa muwakilishi wa blog
hii nchini Malawi ambae pia ni reporter wa Dw, viongozi hao bado walikua wanahojiwa
na kitengo cha interejensia katika makao makuu ya jeshi la polisi Nchini Malawi,
Imbukwe
kwamba chama hicho za MCP na PP cha Joyce Banda wiki zilizo pita walimpa siku
90 rais wa Malawi Mutharika ambaye ni Profesa wa sheria na ni mwana sheria na
mukufunzi wa wana sheria na blog hii ilitoa habari hiyo,
Mutharika
amewahi kua muhadhiri katika Chuo kikuu cha UDSM Nchini Tanzania mwaka 1966
hadi 1969
Rais
Mutharika kazaliwa mwaka 1940 katika wilaya ya Thyolo kijiji cha Chisoka Nchini
Malawi na lakini maisha yake kwa muda mrefu amekua akifundisha katika vyuo
mbali mbali Nchini Marekani.
Wakati
huo huo kuna fununu kua wabunge wa bunge la Malawi wa nasubiri kupewa posho zao
za kujikimu (allowances) ambapo wanaelekea kwenye mukutano wa bunge hilo ambao
unaanza juma hili.
Kwa kawaida
ya bunge la Malawi, wabunge wanapewa hela zao za kujikimu juma moja kabla ya
siku ya kuanza mkutano.
Wananchi
wa Malawi na mashirika yasio ya kiserikali wanangalia kwa makini kama wabunge
watatoa michango yawo kwa uweledi au watakua wakipinga kila jambo.
Wabunge
wa Malawi wamekua na tabia ya kususia vikao kwasababu ya kuto pewa posho za
vikao kwa mda mwafaka au kua mdogo.
Wabunge
wengine hawajapata taarifa kamili kutoka ofisi ya bunge kama posho zao
zitachelewa au laa.
Wabunge wa Malawi kila moja anapewa kwacha 40,000 (US$53) na K10, 000(US$13.2)
kwa kila siku wanapohudhuria vikao.
Lakini
tarifa kutoka katika ofisi ya spika wa bunge hilo zinasemea maandalizi ya kuwalipa
wabunge ya naendelea.
Kuna
hofu kubwa kutoka kwa wananchi kwamba huenda wabunge wataweza kususia vikawo
hivo.
Kipindi
cha utawala wa rais Mutharika ambae ni marehemu, aliondoa viposho visivo na tija,
kwa madai kwamba ni uharibufu wa fedha za walipa kodi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni