Kwa
mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), vifo zaidi ya milioni moja
husababishwa na malaria katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara
Malaria
hayo husababishwa na mbu jike aina ya anopheles ambao wana tabia za ajabu,
kwani wanachagua nani wa kumng’ata na yupi hafai kung’atwa, na hapa ndipo
utapata picha kwanini wakati mwingine mnaweza kua mmekaa sehemu watu zaidi ya
mmoja na wachache ndio wakalalamika kushambuliwa zaidi na mbu?,
Kitaalamu
inaelezwa kuwa kuna makundi zaidi ya 3,500 ya mbu duaniani na kati ya hayo
mengi yanajilisha yenyewe kupitia mwili wa binadamu
Mbu
maarufu zaidi ni jike aina ya anopheles ambaye haumbukiza malaria, kwa kawaida
mbu huyu hutegemea mimea kujilisha, lakini anahitaji viini lishe vilivyomo
kwenye damu kwa ajili ya kutaga mayai na kuzaliana,
Dr.
Fredos Okumu, ni mwanasayansi na mtafiti wa kitengo cha Afya ya Mazingira
katika Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) anasema ni kweli kuwa mbu wana tabia ya
kuchagua mtu wa kumuuma kwani wana uwezo wa kunusa na kutambua harufu, unyevu
joto
la mwili, lakini zaidi hasa harufu kwani kila mmoja na harufu yake.
Anasema
Dr. Okumu kuwa mwili wa binadamu huzalisha kemikali tofauti zaidi ya 500 ambazo
nyingi kati ya hizo hutambuliwa kwa urahisi na mbu kwa kutumia antenna mbili
zilizo vichwani mwao, Tafiti zinaonyesha kuwa mbu wanavutiwa zaidi na harufu za
mwili zitokananzo na tindikali aina ya Lactic na ile ya uric na harufu ya
pombe.
Kemikali
hii ni Lactic hutolewa nje kupitia vitundu vidogo katika ngozi na huzalishwa
baada ya mazoezi,
Wakati
huohuo, kemikali ya uric huzalishwa katika mkojo lakini harufu yake hutolewa
kwa njia ya ngozi pia, harufu ya octenol hupatikana wakati mtu anapohema au
kutoa jasho, hivyo kama unahema kwa nguvu, unazalisha octenol zaidi na
kuwavutia zaidi mbu.
Dr.
Okumu anasema baadhi ya watu huzalisha kemikali hizi kuliko wengine, hivyo
uwezekano wa mbu kuwafuata ni mkubwa zaidi. Na kwamba utafiti uliofanywa na
jopo la madaktari (Profesa Niels O. Verhulst na wenzake) katika chuo kikuu cha
Wageningen, Uholanzi umeonyesha kuwa mbu wanavutiwa na aina ya bacteria ambao
huishi katika mwili wa binadamu
Utafiti
huo wa mwaka 2011 katika maabara ya tabia za mbu (entomology) umeonyesha kuwa
mtu anaweza kuwa na baktereia ambao hawawavutii mbu na mwingine ana bacteria
ambao ni kivutio cha mbu,
Utafiti
umebaini kuwa pamoaja na tabia nyingine mbu hupenda zaidi wanawake kwa kuwa hao
hupenda kuachia miili yao wazi kuliko wanaume,
Marta
Maia, Mtafiti wa Tabia za Mbu wa Kitengo cha Afya cha Ifakara, kituo cha
Bagamoyo anasema ni tabia ya mbu kuchagua nani wa kumng’ata na nani wa kumwacha
kutokana na kinachowatia
Mbu
huvutiwa zaid na ukubwa wa joto la mwili, hivyo watu wanene,harufu ya mwili na
hewa ya kabonidayoksaidi, ambapo anasema kuwa mbu huvutiwa zaidi na wanawake
wajawazito kutokana na mabadiliko ya vichocheo na uzito wa mwili,
“mbu
hupenda zaidi wanawake wajawazito kwa sababu huwa na uzito mkubwa zaidi na joto
la miili yao huwa kubwa zaidi na miili yao huwa na virutubisho zaidi,”
Mtaalamu
wa Tabia za Mbu, Dk. James Lofan wa shule ya Mazingira na Tiba za Magonjwa
yasabishwayo na hali ya hewa anasema mbu wana njia kadhaa za kuwinda mlo wao
mojawapo ikiwa ni aina ya maumbo yetu na hewa chafu tunayopumuam Dk. Logan
anathibitisha kuwa watu wenye uzito mkubwa wana tabia za kuiacha miili yao wazi
hivyo mbu hupata nafasi ya kuwauma.
Lakini
huwafuata zaidi wanawake wajawazito si kwa sababu ya ongezeko la uzito pekee,
bali kwa sababu ya mabadiliko ya vichocheo wayapatayo wajawazito husababisha
wawe na joto la juu na uzalishaji mkubwa wa hewa chafu,
Dr.
Dube Ncube wa Hospitali ya Rosebank, kitengo cha Malaria nchini Afrika Kusini
anasema, mbu hutumia zaidi ogani iitwayo maxillary pal kunusa harufu ya hewa
chafu kabla ya kwenda kwa mlengwa kufanya mashambulizi
Ogani
hii ni makini mno kwani inaweza kunusa harufu ya hewa chafu kwa umbali wa futi
160, laini pia utafiti uliofanywa nchini Japani kwa vijana 13 ulibaini kuwa
wanywaji wa bia huumwa zaidi na mbu kuliko wasiotumia kilevi hicho, alisema mbu
huvutiwa na wanywaji wa pombe kwa kua pombe humfanya mtu kutokwa zaidi na jasho
ambalo ndani yake limetawaliwa na harufu ya pombe hivyo kuwavutia zaidi mbu.
Kundi
la damu
Dr.
Meshack Shimwela, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Hospitali ya
Amana jijini Dar es salaam anasema mbu huvutiwa zaidi na damu za kundi O
Watu
wenye damu ya kundi O huumwa zaidi na mbu kulilo watu wa kundi A, “hizi ni
tabia za mbu zinazowafanya wabutiwe na harufu fulani za mwili na aina ya kundi
la damu, “ni kama binadamu anavyopendelea chakuala hiki na kukichukia kile”
anasema Dr. Shimwela, Nae Dk
Emmanuel
Kaindoam mtafiti na mwanasayansi katika Taasisi ya IHI anasema mbu pia wana
tabia ya kupenda nyumba zenye watu wengi, wanene na wazee
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni