Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imetoa rai kwa viongozi wa
mikoa na wilaya, wataalamu na wanajamii kutoficha taarifa ya ugonjwa wa
kipindupindu kwani kufanya hivyo kunakwamisha juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo
nchini.
Aidha
wizara hiyo i mesema kwamba yenyewe ndiyo yenye jukumu la kutoa taarifa za
ugonjwa huo,hivyo mtu mwingine akitoa taarifa ni zake binafsi .
Kauli
hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla, wakati akitoa taarifa ya wiki kuhusu ugonjwa wa
kipindupindu nchini kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara
hiyo.
“Moja ya changamoto kubwa inayoendelea
kujitokeza ni pale ambapo baadhi ya wataalamu wa ngazi mbalimbali pamoja na
wanajamii wanapoficha wagonjwa na hivyo kutoa taarifa ya wagonjwa wachache
kuliko uhalisia.“ Madhara yanayoambatana na hii ni kutokuwepo kwa taarifa za
kutosha zitakazo ongeza juhudi za kuzuia ugonjwa kutoka katika maeneo ambayo
wagonjwa hawakutolewa taarifa na hivyo kuongeza hatari ya ugonjwa kuendelea
kusambaa kimnyakimnya na baadae kusababisha wagonjwa wengi kujitokeza katika
maeneo hayo kwa maramoja,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Aidha
Dkt.Kigwangalla alitoa rai kwa viongozi wa hususan ngazi za mikoa na wilaya
kutokutoa kauli za kutaka kuwaadhibu watendaji na viongozi wa ngazi za chini
kwa kigezo cha wagonjwa kuwepo katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo
wataongeza kasi ya kuficha wagonjwa na kumwamisha juhudi za kupambana na
ugonjwa huo.
“Sisi tutaendelea kutoa taarifa za ugonjwa
huu, hata kama hawataki kukubali kama kuna kipindupindu, tunafanya hivyo kwa
sababu tuna takwimu sahihi,kama hawataki kutumbuliwa majipu sisi tutayatumbua,”
alisema.
Naibu
Waziri huyo alifafanua hayo kufuatia baadhi ya viongozi kudai Jiji la Dar es
Salaam halina mgonjwa wa kipindupindu baada ya vyombo vya habari kuripoti jiji
hilo lina ugonjwa huo na wagonjwa waliokuwepo ni sita kwa mujibu wa taarifa za
wizara hiyo za wiki iliyopita.
Katika
taarifa hiyo ya wiki kuanzia Februari 15 hadi 21, mwaka huu, Dkt. Kigwangalla
alisema jumla ya wagonjwa walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni 499, ambapo kati
ya hao wagonjwa sita (6) walipoteza maisha.
Alisema tangu ugonjwa huo ulipoanza Agosti mwaka mwaka
jana hadi sasa jumla 16,352 wameugua ugonjwa huo, kati ya hao 249 wamepoteza
maisha. Aliongeza kwamba kwa kipindi cha wiki hiyo, jumla ya mikoa 11
imeripotiwa kuwa na ugonjwa huo, ambapo mkoa wa Iringa ndio unaongoza kuwa
idadi kubwa ya wagonjwa 143, Mwanza 94, Mara 87, Dodoma 66, Morogoro 42,Mbeya
30,Arusha 17,Dar es Salaam 14,Simiyu3,Kilimanjaro 2 na Manyara 1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni