Polisi ya India imesema
mwanamme mmoja aliefahamika kwa jina la Hasnin Anwar Warekar mwenye umri wa miaka 35 ameuwa watu 14 wa
familia yake kwa kuwachinja kwa kisu na kisha yeye mwenyewe kujiua.
Saba miongoni mwa
wahanga wa mauaji hayo yaliyotokea karibu ya mji mkuu wa kibiashara nchini
India, Mumbai ni watoto wadogo.
Polisi imesema muuaji
huyo Hasnin Anwar Warekar amewauwa jamaa zake walipokusanyika katika nyumba
moja jana Jumamosi. Warekar aliwachinja watu hao, wakiwemo wazazi wake, na
baadaye akajinyonga kwa kamba.
Kwa mujibu wa taarifa
za uchunguzi wa awali, Warekar aliweka dawa ya kudhoofisha mwili kwenye chakula
walichokula watu wa familia yake, na kisha akaanza kuwachinja mmoja mmoja baada
ya kulala.
Dada yake mmoja mwenye
umri wa miaka 21 ambaye amenusuriwa na majirani, anatajwa kuwa katika hali ya
mshituko mkubwa.
Bado kuna utata kuhusu
sababu iliyomfanya Warekar kufanya mauaji hayo, lakini inadhaniwa imetokana na
mzozo kuhusu mali ya kifamilia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni