Askofu Martin Mtumbuka wa Jimbo la Kusini mwa Malawi Karonga |
Askofu wakanisa la katoliki diocese ya
kusini mwa Malawi Martin Mtumbuka amesitisha michango na sadaka zingine ambazo
wawumini wa kanisa hilo walizokua wakitoa.
Askofu Martin Mtumbuka alitoa agizo hilo
wakati alipokua katika wilaya ya Karonga katika kanisa la St Mary's wakati wa balaza
kuu la kanisa hilo lililo fanyika mwisoni mwa wiki iliyo pita.
Mtumbuka alisema kwa sasa nchi ya Malawi
imekumbwa na janga la chakula na watu wana poteza muda mwingi kushinda katika
vituo vya kuuzia mahindi.
“Nafikili hatakua jambo Njema kwa
mwenyezi Mungu kwamba watu waendelee kutoa hela kasini wakati kwa sasa nchi
inajanga la chakula kama hivyo kanisa tuna amini watu wenye afya nzuri ndio
pekee wanawoweza kujenga kanisa, ni majukumu yetu sisi viongozi wa dini kua nchi
inakua na watu wenye afya njema, elimu, haki, na amani, alisema asikofu
Mtumbuka.”
Katika hutuba yake Mtumbuka alinukuliwa
na mwandishi wa habari hii ambae pia ni muwakilishi wa blog hii nchini Malawi akisema
jukumu la kuhakikisha kwamba watu wanakua na chakula cha kutosha sio la kuiachia
serikali peke yake ila ali ni jukumu la
kila mtu, wakiwemo viongozi wa dini, na alisihi kila kiongozi kuchukuwa hatua haraka ili
kukabiliana na janga hilo,
Pia kiongozi wa kanisa hilo alifutilia
mbali michango ya ibada ya '' Paper Sunday na michango ya siku kuu ya khrimasi
nakuwasihi wawumini wa kanisa hilo hela waliyotakiwa kutoa kwenda kununua
chakula cha kutosha na kufanya kazi za shambani kwa bidii ili kuepukana na
janga hilo.
Mwaka jana nchi ya Malawi ilikumbwa na
mafuriko ya maji ambapo mazao na mashamba ya wakulima yalitoweka na maji Kutokana
na hilo imesababisha inchi ya Malawi kua na baa la njaa,
Wilaya ya Nkhata-Bay iliyo pembezoni maziwa
la Malawi inasemakana wana nchi wengi wana chakula Kutokana na kwamba wengi ni
walilima kwa wingi zao la mihogo na kwamba unga wa muhogo umekua ukitumika sana
na kwa sasa wilaya hio imekua msaada kwa wilaya zingine kwa kutoa msaada wa
chakula. Chakula kikubwa nchini Malawi
ni ugali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni