Jumatano, 3 Februari 2016

Wanafunzi hatarini kubomokewa

Diwani wa kata ya Lutemba bw. Imanuel Ghoba

Baadhi ya majengo ya shule ya msingi Lubala
moja ya jengo la shule ya msingi Lubala
Baadhi ya majengo ya shule ya msingi Lubala
Wanafunzi wa shule ya msingi Lubala iliopo kijiji  cha  Luteba   kata ya Luteba Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wako hatalini kubomokewa na majengo ya shule hiyo kutokana uchakavu wa baadhi ya majengo hali ambayo imelazimu baadhi ya majengo kuegeshwa kwa miti.

Wakiongea kwa masikitiko makubwa baadhi ya wanafunzi shuleni hapo kwa sharti la kutotajwa majina walisema hali ya hofu hutanda zaidi miongoni mwao pindi mvua inayo ambatana na  upepo inapo kuwa ikinyesha kwa kua baadhi ya majengo yamekua yakitikisika hali inayopelekea wanafunzu kupoteza usikivu wakati wa masomo kwa hofu ya kuangukiwa na majengo,

Wanafunzi hao wamesema hali hiyo imekua ikidhoofisha uwezo wao kitaaluma kutokana na kupoteza umakini wa kusikiliza kile ambacho hufundishwa hata wakati wa kujisomea hivyo wameiomba serikali kulitazama suala hilo kwa jicho la ziada kwa maslahi ya usalama na taaluma yao.

Mmoja wa wananchi aliejitambulisha kwa jina la Elia mwalisu alisema, hali ya uchakavu katika shule hiyo inatishia amani na kwamba hali hiyo imedumu kwa miaka kumi sasa.


Mwalisu amesema kua hali hiyo inatishia usalama wa watoto na kuathiri uwezo wa wanafunzi kitaaluma hususani katika kipindi hiki ambacho mvua kubwa zinanyesha mfululizo hivo kuwataka viongozi wenye dhamana kutatua hali hiyo.

Aidha mwananchi huyo aliongeza kwa kusema licha ya majengo kuwa mabovu na kuegeshwa kwa miti lakini  baadhi ya walimu shuleni hapo wamekuwa wakivuna mahindi na kisha kufunga kwenye makenchi ya majengo jambo ambalo ni hatari zaidi.

Diwani wa kata  hiyo Imanuel Ghoba Mwaibupungu , amekiri kuwepo kwa baadhi ya majengo ambayo yapo hatarini kubomoka kutokana na uchakavu ambapo alisema wapo katika mkakati wakufanya ukarabati wamajengo uongozi kwa ngazi ya wilaya walifika shuleni na kuahidi kusaidia katika ujenzi baada ya kupewa taarifa.

Afisa elimu shule za msingi wilayani humo Jeni Mwakapalala, ambae mbali na kukiri kuwepo kwa adha hiyo, alisema walifika shuleni hapo na kuahidi kufanya ukarabati shuleni.

“tupo kwenye mkakati wa ujenzi wa madarasa ya shule hiyo na baada ya kupata taarifa tulifikaeneo  la  shule na kujionea halihalisi, hivyo katika mipango yetu ya mwaka 2016  hilo nalo tumelipa kipaumbele zaidi”. Alise mwakapalala.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni