Hii
ni habari njema kwa wazazi wote wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya
vichwa kujaa maji au watoto waliozaliwa na matatizo ya mgongo wazi.
shirika
la FOCC Friends of children with cancer wamejitolea kutoa huduma ya upasuaji na
uchunguzi kwa watoto wote wenye dalili kama hizo na wale wanaozaliwa na
matatizo hayo madaktari wa shirika hili wapo katika hospitali zote za rufaa
Tanzania zikiwemo Bugando Mwanza, Rufaa Mbeya, Mhimbili Moi, KCKC Moshi.
Ni
wakati sahihi kupunguza matatizo hayo pia wakinamama wanashauriwa kufuata
taratibu za lishe bora wakati wa ujauzito ili kuepuka kuzaa watoto wenye vichwa
kujaa maji na mgongo wazi.
Uchunguzi
na tiba vitafanyika 04-05 /02/2016 kwa wakaazi wa mbeya Tanzania na nyanda za
juu kusini katika hospitali ya rufaa Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni